Je hii inaeleweka?

Si hivo Alter, Hapa tunaongelea couple imesha kwaa kwa muda na mmoja anaona it is time to move to the next level, mwenzie anamwambia hawezi kurupukia mahusiano ya kudumu. Unaona hapo?
Hii ndio nilikuwa nafikiri. Kwa nini achukue muda wote huo kulisema hilo, asiseme tangu dakika za mwanzo na yule mwengine akaelewa angalau akae mkao gani.
Anyway, better late than ever! Salama hakutamka hivyo baada ya kuzaliwa mtoto mmoja.
 

...once bitten, twice shy, thrice?...celebral malaria!


...pamoja na majibu mazuri ya wachangiaji waliotangulia, ningeomba kumuuliza MwanajamiiOne mahusiano ya kudumu ana maanisha nini? hapa amekusudia ni ndoa?

...kama jibu ni ndio, nyie endeleeni na mdahalo huu kwani mbu nishajipatia uzoefu wa kutosha kwenye taasisi hii kwamba happiness haipo kwenye ku fremu cheti cha ndoa pekee...otherwise tungesikia huyu ana diploma ya ndoa, yule ana degree, wale wana Masters, au waliokufa na Phd za ndoa...

Ndoa utajitahidi sana utaishia ngazi ya cheti kama sio kupigwa "disco" kama kina mbu hapa.
MwanajamiiOne, mahusiano ya kudumu unakusudia nini, ndoa?



 
Nyie watu mbona mnanishambulia as if ni mie ndo nmeambiwa maneno hii loh hahahahaha nimeuliza tu.
 

Mbu aksante kwa mchango huu. Ni kweli namaanisha ndoa na hasa kwa wale ambao hawsajawahi ingia kwenye taasis hiyo.
Tunajua fika kuwa jamii zetu wazazi wetu huwa wanakuwa na matumaini mengi kwa watoto wao ikiwemo kuwa0za nao wawe na familia zao.

Sasa unapokuwa unahisi kuwa umempata the right person na unajiona ni muda muafaka sasa nawe uwe na familia yako unapomweleza mwenzako ambae unahisi ndo anaweza kuwa your better half, akupe majibu hayo!
 
Aksante Lizzy hahah umenifurahisha maana ulivyolirukia swali la The Boss hadi nimependa!
 
Sasa mwali wewe, bora umewahi kujitetea kuwa sio wewe! Manake ushaambiwa mwenzio hana mpango wa kutoka kwenye gereza alilofungiwa japo kwa kuruka ukuta, ww unategemea ataamka siku aseme twende tukapunge upepo? Ukishaambiwa hivyo inamaanisha bado nipo nipo sana...
 

Shost nimeona mashambulizi yanaletwa direct nkaogopa nisijechakachua michango ya watu loh!

MJ1 na uzee huu ? Naanzia wapi mie kubembeleza tuunge undugu na mtu! Nshajiondokea mie huko! Nawasaidia tu wadogo zangu wa leo.

Na kweli mwaya so mtu ndo ashakupa za uso hizo, ndo unamweleza wazi kuwa kama ni hivyo haya endelea kuuguza makovu yako, mie nendatafuta alokwishasahau kuwa ana makovu (unaanza mbele na kuanza moja kupenda mwingine) au ndo unajipa moyo kwanza kuwa pengine hayo maumivu ya makovu!! Yataisha muda si mrefu (umsubirie?) Au ndo unafanyaje vile???
 
He/she means that you should keep one door open for the rainy day.......
 
Hivi kwa nini kisianzishwe chuo cha kufundisha mahusiano? Its the most complex thing even known to human kind.

Wanasayansi wanarusha roketi kwenye space lakini wamepigwa chini na wenza wao au wameumizwa. Ndo maana Newton hakutaka jihusisha kabisa na mahusiano.

Unajua mtu anaweza akakujibu kama alivyosema MJ na still ukashindwa kumuacha.

Nachoamini ni kuwa hauuambii moyo feel this. Wakati mwingine kabisa unajua uko kwenye temporarly relationship na kila mtu anatafuta right candidate na bado ukajikuta unaanza mfeel huyo mtu.

japo wanasema mapenzi tni try and errors hadi utakapompata the right person lakini kama hutaki kuumia bora ukae mwenyewe.
 
Aksante The Boss, what if mmekaa muda ambao unahisi unatosha kwa kumove to the next step?! Mara nyingi hii hutokea mnapokuwa mmekaa kwa muda kiasi
Muda haupangwi na wewe mda unapangwa na mtekelezaji!!
 
Hayo mambo yenu vijana endeleeni ngoja niende kule kwa wazee wenzangu
 

Shida inayoonekana hapo ni kuusemea moyo wa mwenzi wako!!

Ni jambo gumu sana....Ila ni hatari kutegemea jibu positive tu kutoka kwa mtu ambaye mmekutana barabarani na kila mmoja akiwa na meno yake 32!!
 
Nimekusoma Mwj1, mshawishi awe mvumilivu....ni taasisi ya kuishi kwa matumaini na vipimo cha uvumilivu.
"mapenzi ni kukubaliana (baada ya ushawishi), mapenzi si kulazimishana!"
Mwenza hajashawishika bado kuchukua maamuzi magumu...
 
Natamani nikuelewe.......... Kukubaliana kupendana?πŸ˜›hoto:πŸ˜›hoto:πŸ˜›hoto:
 
The great part kuhusi hilo ni walau S/he is telling you the truth na NO empty promises, sema tu watu twapenda jisikia we are the center ya maisha ya mtu alo mpenzi wako; hoping akuambie maneno kama "bila wewe hawezi ishi...." hata kama sio kweli...

well said mamito


Afadhali umepooza moyo wangu hapo lol.
 
Nimekusoma Mwj1, mshawishi awe mvumilivu....ni taasisi ya kuishi kwa matumaini na vipimo cha uvumilivu.
"mapenzi ni kukubaliana (baada ya ushawishi), mapenzi si kulazimishana!"
Mwenza hajashawishika bado kuchukua maamuzi magumu...

Aksante Mbu so inatubidi tuvumilie na kuishi kwa imani loh! Tatizo ni kuwa kwa wadogo zetu wa sasa mpaka inafikia mtu anakuuliza swali linalopelekea kujibiwa hivi ni tayari weshaanza kuishi pamoja! Sasa ndo unavumilia na bado mwisho wa siku unaambiwa, nadhani sitowezaolewa na wewe; siko tayari kukuoa wakati kipindi ulishaambiwa bado anaugulia maumivu! Mwe
 
Natamani nikuelewe.......... Kukubaliana kupendana?πŸ˜›hoto:πŸ˜›hoto:πŸ˜›hoto:

Nyie nanyi kwa kujifanya walimu wa lugha! Kwani ulipompenda Bibi si ulimweleza naye akakukubali kwa kuwa kakupenda pia? Mnaamua sasa tupendane au huwa inakuwaje wajameni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…