Jaluo_Nyeupe
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 2,824
- 2,264
Salaam wana JF.
Siku kadhaa zilizopita nilitangaza hapa JF kwamba natafuta mchumba. Siku moja nikiwa kwenye gari nilipokea simu ya dada mmoja nisiyemfahamu na wala hakutumia namba za simu nilizoziweka hapa. Akasema yeye ana shida anatafuta mchumba na alikwenda kwa mchungaji wa kanisa lao akamuombea na kuahidiwa atapata mchumba kwa njia ya mawasiliano ya simu, sasa katika kubonyeza bonyeza simu yake mara akajikuta ameandika namba zangu.
Kinachonishangaza kwa huyu binti haraka aliyonayo, hatuwahi hata kuonana lakini tayari anasema ananipenda sana, kuniomba nimtumie vocha na kutaka tuonane bila hata kunipa muda wa kujadili kile anachokisema. Sasa wana JF mnanishaurije, hii inaweza kuwa ni bahati na kwamba maombi yangu yamejibiwa au ni mbinu mpya za kiutapeli zimeingia hapa jijini?