Je hii ni bahati au utapeli?

Je hii ni bahati au utapeli?

Jaluo_Nyeupe

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
2,824
Reaction score
2,264
Salaam wana JF.

Siku kadhaa zilizopita nilitangaza hapa JF kwamba natafuta mchumba. Siku moja nikiwa kwenye gari nilipokea simu ya dada mmoja nisiyemfahamu na wala hakutumia namba za simu nilizoziweka hapa. Akasema yeye ana shida anatafuta mchumba na alikwenda kwa mchungaji wa kanisa lao akamuombea na kuahidiwa atapata mchumba kwa njia ya mawasiliano ya simu, sasa katika kubonyeza bonyeza simu yake mara akajikuta ameandika namba zangu.

Kinachonishangaza kwa huyu binti haraka aliyonayo, hatuwahi hata kuonana lakini tayari anasema ananipenda sana, kuniomba nimtumie vocha na kutaka tuonane bila hata kunipa muda wa kujadili kile anachokisema. Sasa wana JF mnanishaurije, hii inaweza kuwa ni bahati na kwamba maombi yangu yamejibiwa au ni mbinu mpya za kiutapeli zimeingia hapa jijini?
 
Jaluo bana unakuwa kama sio mtoto wa mujini.. we tuma vocha tu umeliwaa matapeli wapo wa aina nyingi siku hizi. Hakuna cha bahati hapo bali ni utapeliii:lol::lol::lol:
 
kimbia mwaya,huyo dada atakuwa amejua labda kupitia rafiki zako hio namba yako amekulia timing tu na probably anajua kupitia hao hao marafiki zako kama uko single na unatafuta mtu,yeye bila haya anataka kutake advantage kuwa uko desperate........hajafunuliwa lolote aache uongo!
anywayz wewe ni mwanaume,unaweza ku hang naye ila kwa akili sana manake huyu amekaa kichunaji chunaji sana hio ya kuomba vocha hata mtu hujamzoea/humjui inaelekea huyu dada anawinda!
 
Man this sounds "iffy":frown:

On the other hand what's life without risks? Mimi nakushauri usikimbie ila hiyo habari ya vocha mpe the business, i.e "U know it just that umenikuta wakati mbaya, blah blah................"then u'll be able know from her reaction
 
Jaluo hebu acha kunichekesha yaani huoni kabisa kama huyo yuko kibiashara zaidi?? Hata hakujui anaomba vocha?? Wewe shituka msala huo hakuna cha kubonyeza namba wala nini huyo ana taarifa zako zote kuwa unatafuta mchumba so anatake advantage.
 
Pole kwanza ndugu yangu kwa wakat mgumu ulio nao. Ni rahs kupata mpenz kuptia internet kama ilvo kwa marafk, inawezekana pia ni utapel unaofanywa na wanaokufaham. Nadhan kubal kukutana nae utaweza mfaham zaid...kwa swala la vocha fuata ushaur wa
 
Pole kwanza ndugu yangu kwa wakat mgumu ulio nao. Ni rahs kupata mpenz kuptia internet kama ilvo kwa marafk, inawezekana pia ni utapel unaofanywa na wanaokufaham. Nadhan kubal kukutana nae utaweza mfaham zaid...kwa swala la vocha fuata ushaur wa nemo
 
Kwani vocha mahela mangapi?
Mtumie ya mia tano uone itakuwaje.
 
Kwani vocha mahela mangapi?
Mtumie ya mia tano uone itakuwaje.

Kama ulikuwepo kwenye bongo langu
Atume Jero tu kwisa habari
Tena mwambie na wewe unampend sana, na ulikuwa unamsubili kwa hamu kweli
Mwambie aje unapokaa fasta

The Following User Says Thank You to Husninyo For This Useful Post:

CPU (Today)​
 
Salaam wana JF.

Siku kadhaa zilizopita nilitangaza hapa JF kwamba natafuta mchumba. Siku moja nikiwa kwenye gari nilipokea simu ya dada mmoja nisiyemfahamu na wala hakutumia namba za simu nilizoziweka hapa. Akasema yeye ana shida anatafuta mchumba na alikwenda kwa mchungaji wa kanisa lao akamuombea na kuahidiwa atapata mchumba kwa njia ya mawasiliano ya simu, sasa katika kubonyeza bonyeza simu yake mara akajikuta ameandika namba zangu.

Kinachonishangaza kwa huyu binti haraka aliyonayo, hatuwahi hata kuonana lakini tayari anasema ananipenda sana, kuniomba nimtumie vocha na kutaka tuonane bila hata kunipa muda wa kujadili kile anachokisema. Sasa wana JF mnanishaurije, hii inaweza kuwa ni bahati na kwamba maombi yangu yamejibiwa au ni mbinu mpya za kiutapeli zimeingia hapa jijini?

Mchumba + Humjuwi + Vocha = Utapeli
 
JALUO hujawahi kupigwa mzinga wa VOCHA wewe???
Mbona simpo sana, fuata ushauri wa HUSNINYO!!!! Tuma 500 inatosha.
 
Jamani tatizo sio kutuma vocha, tatizo ni speed anayokuja nayo ndio inanitisha na kunipa wasiwasi. Hataka hata tuchat zaidi tufahamiane, yeye anachotaka ni nimwambie naishi wapi anifuate. Ingawa hatuishi mbali mbali sana lakini nahofia kumwambia mapema mapema waweza kukutana hata na jini.
 
Kama ulikuwepo kwenye bongo langu
Atume Jero tu kwisa habari
Tena mwambie na wewe unampend sana, na ulikuwa unamsubili kwa hamu kweli
Mwambie aje unapokaa fasta

The Following User Says Thank You to Husninyo For This Useful Post:

CPU (Today)​

Duh! we hunitakii mema kabisa, na je akija kweli ukakuta hakufai utaanzaje kukimbia na ulishamwambia kwamba nawe unampenda?
 
JALUO hujawahi kupigwa mzinga wa VOCHA wewe???
Mbona simpo sana, fuata ushauri wa HUSNINYO!!!! Tuma 500 inatosha.

Nimewahi mara nyingi tu mkuu, lakini kwa ninayemfahamu sio kutuma tu ukute unamtumia dume mwenzako.
 
Hahahaaa, wengine huwa wanasema simu yake inaweza kuzima akiweka vocha za jero.

wewe unahitaji mke. Mke ni lazima awe heshima.
Mdada mwenye dharau ukishamtumia vocha ya jero au ukimpunguzia 250 utaiona dharau yake.
Jaribu utaniambia...
 
Back
Top Bottom