Je hii ni bahati au utapeli?

Ndio maana siungi mkono sana, haya matangazo ya kutafuta mchumba.
Bora mtu ukajichanganya na watu humu, ukasoma post za watu, utajua tu huyu ni single huyu ni hivi then una ongea kirafiki, huwezi jua kesho bwana, maisha yanaweza kuwa zaidi ya keyboad, zaidi ya urafiki na zaidi ya undugu pia.

Sio matangazo kama unatangaza nafasi za kazi. Ndo hayo matokeo yake.
 
Ebwanae huyo si mwanamke, mwanamke gani cku ya kwanza tu anaanza kukupga mizinga na kudai anakupenda mwanamke gani hata aibu za kike hana?
 
Hahahahahahahah
kuna raha sana Jf
Alijuaje na we ni single na unatafuta?

ANGALIA USIJE OA JINI Mpenzi..

Hapo ndipo napaogopa zaidi, bora awe tapeli mwenye shida ya vocha tu kuliko jini mahaba.
 


Wakati mwingine ni vizuri kutoa tangazo ili hata kama inatokea mnachat na mtu hapa JF aliyeku-PM mnakuwa na nia moja wote kuliko kum-PM mtu tu ili mradi umeona yupo single. Unaweza ukapoteza muda mrefu kufahamiana na mtu utakapoamua kumweleza nia yako kumbe mtu tayari ana rafiki au mchumba wake.
 
Mbona simpo tu!!mtumie buku ili kama alikopa kwenye mitandao yetu abakiwe na chenji,kisha msikilize huenda ni taperi but huenda akakufaa pia
 
Cha mjinga huliwa na mwerevu kaka, Sijekatuma vocha wala nini tulia na bahati yenyewe itajondea bila kuangaika.
 
angalia sifa unazotaka ametumia,kuwa makini kuchunguza tabia je anamtazamo sawa na ww ktk maisha.ukiridhika kuwa naye
 
angalia sifa unazotaka ametumia,kuwa makini kuchunguza tabia je anamtazamo sawa na ww ktk maisha.ukiridhika kuwa naye.ila kuwa makini asijekuwa ni kibiashara zaidi
 
Mbona simpo tu!!mtumie buku ili kama alikopa kwenye mitandao yetu abakiwe na chenji,kisha msikilize huenda ni taperi but huenda akakufaa pia
ahahahaaa! Kwa hiyo ukituma jero inaweza kuishia kwenye makato...LOL!
 
angalia sifa unazotaka ametumia,kuwa makini kuchunguza tabia je anamtazamo sawa na ww ktk maisha.ukiridhika kuwa naye.ila kuwa makini asijekuwa ni kibiashara zaidi
Ni kweli......ila swali nalojiuliza hadi leo alipataje namba zangu?
 
pole sana kwa "bahati" uliyopata. uchumba ni nini? nini kinaanza? nini kinafuata? je mazingira gani yanahusiana na matokeo ya uchumba.
haya ndio mazingira yanayoweza kukufanya ukawa na mahusiano ya muda mrefu yenye matokeo mazuri.
kumpenda mtu si mpaka umuone japo utakapo muona unaweza kubadili mawazo kwani mtazamo wako unaweza kuwa kwenye mvuto wa maongezi yakakupa picha kuwa mtu huyu nadhani acha tu. ukimuona ukaona vigezo vya maongezi havifanani na maumbile ukakimbia.
je hii ni bahati? nadhani lazima ujue unatafuta nini kwanza japo mapenzi ambayo ndiyo yanajenga uchumba na baadaye ndoa yanaweza yasikupe nafasi kabisa ya kujadili laki kuwepo na vigezo ambavyo binaadamu yoyote mwenye akili timamu atasema hata mimi ningefanya hivi.
nadhani kwanza muonane au umuone ndipo useme kuwa umeona na umehitaji. chunguza ni binadamu wa aina gani kama kukupigia tu kaanza kuhitaji na salio je yuko na mahitaji gani japo kuomba salio si kigezo sana katika hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…