Je hii ni dalili mwananchi wa kawaida kashachoka?

Je hii ni dalili mwananchi wa kawaida kashachoka?

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
5,565
Reaction score
843
Atinga na kisu bungeni
Selemani Mpochi
Askari polisi mwenye namba E 5420 Hassan Ngoma, ambaye yupo katika kikosi cha Polisi Bunge, jana alinusurika kuchomwa kisu na kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Kwa mujibu wa askari huyo, kijana huyo aliwasili eneo la nje la uzio wa Bunge ambako kuna lango kuu la kuingilia magari ya viongozi saa 6:00 mchana na kuanza kupiga kelele huku akionyesha nia ya kufanya fujo eneo hilo.
"Baada ya kuona kuwa kijana huyo ataondoa utulivu uliopo eneo hilo, niliamua kwenda kumtuliza, ndipo alipochomoa kisu na kutaka kunichoma, nilikwepa kwa kurudi nyuma, lakini kijana huyo alizidi kunifuata hadi nilipofika lango la kuingilia magari," alisema askari huyo.
Alisema muda wote kijana huyo alikuwa ameshika kisu mkononi akitaka kuchoma mtu yeyote aliyekuwa mbele yake.
Alisema mbele ya lango hilo kuu, kulikuwa na askari wengine.
Wakati mkasa huo ukitokea, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alikuwa anakaribia kujibu hoja mbalimbali za wabunge waliokuwa wamechangia hotuba ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2009/10, huku mawaziri wa nchi wa ofisi hiyo, wakijibu baadhi ya hoja za wabunge.
Kwa kawaida, lango hilo hulindwa na askari wa Usalama wa Taifa, Polisi na askari wa kampuni binafsi, lakini wote walitawanyika baada ya kijana kuibuka akiwa katika hali hiyo.
Kijana huyo alifanikiwa kupita kwenye lango hilo na kuelekea kwenye viwanja vya Bunge ndipo askari polisi Ngoma alikwenda kuchukua bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) na kumfuata kabla hajafika kwenye lango linalotumiwa na wabunge kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge.
Kabla hajafika mbali, askari wa Usalama Barabarani ambaye huongoza msafara wa Waziri Mkuu, Ali Ayoub, alimfuata kijana huyo na kumtuliza ili arudi getini.
Baada ya kuona anafuatwa na askari mwenye bunduki, ghafla alimzunguka zunguka askari huyo kwa nia ya kumfanya awe ngao yake endapo polisi mwenye bunduki angemfyatulia risasi.
Mtafaruku huo uliendelea kwa muda wa dakika 10 lakini polisi walifanikiwa kumdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.
Aliondolewa eneo hilo na kuingizwa ndani ya gari la polisi na kumpeleka kituo kikuu cha polisi mkoani hapa.
NIPASHE
Main.jpg


Najua kijana huyu hakupaswa kufanya alicho fanya. lakini kukaa na kufikiri nikawa naona je hizi ni dalili ndogo ndogo kuwa wananchi wa kawaida wameshaanza kuchoshwa na uongozi wetu? Kama mwananchi wa kawaida kajitolea muhanga kufanya kitu kama hicho kwenye jengo analo jua viongozi wapo na kutakuwa kuna lindwa sana ni anajaribu kupaza sauti yake ambayo viongozi wetu hawataki kusikia? Mh tusipo angalia tunaenda kubaya. Anaweza tu kuwa mhuni wa kawaida lakini pia anaweza kuwa kiashiria cha dalili ya watu kuchoka.
 
Huyu ameonyesha kuwa Bungeni hakuna Jipya zaidi ya yale yale na sio Chizi huyu angesikilizwa shida yake na kujua. Ndio MWananchi Wamechoka na Utawala unaoshikiana na Mafisadi.
 
It could be anything, labda kuna mnene anamlia mkewe au bintiye au kuna mzito kamuacha huko shamba na ng'ombe wake kwa miezi mitatu bila kumlipa senti tano au kuna jitu na jitambi lake limekunywa bia na kula kuku kwenye kagrocery kake likaondoka bila kulipa au ana matatizo ya akili baada ya kufyatuliwa na bangi au 'kachezewa', etc- you can make thousands of assumptions! Ni yeye mwenyewe tu ndo anajua kilichompeleka hapo na kuamua kufanya hicho alichofanya, tusikimbilie kuingiza siasa kila mahali.
 
It could be anything, labda kuna mnene anamlia mkewe au bintiye au kuna mzito kamuacha huko shamba na ng'ombe wake kwa miezi mitatu bila kumlipa senti tano au kuna jitu na jitambi lake limekunywa bia na kula kuku kwenye kagrocery kake likaondoka bila kulipa au ana matatizo ya akili baada ya kufyatuliwa na bangi au 'kachezewa', etc- you can make thousands of assumptions! Ni yeye mwenyewe tu ndo anajua kilichompeleka hapo na kuamua kufanya hicho alichofanya, tusikimbilie kuingiza siasa kila mahali.

Ebo!
Kimsingi yote uliyoyataja ni matokeo ya siasa mbovu. Sasa kuna ubaya gani kuingiza siasa katika tukio husika?
 
Mimi sikubaliani na wote hapo hapo juu! nadhani tuipe muda polisi iweze kuchunguza kwani pengine anamagonjwa ya akili!
Tanzania ni moja ya nchi ambazo wagonjwa wa akili hawaangaliwi kwa ustadi maalum, matokeo yako watu wenye matatizo hayo wanajazana mahabusu badala ya kuwasaidia.

Mimi nadhani kabla ya kutoa michango yetu tusubilie uchunguzi yakinifu na wakisayansi ufanyike kwanza...lakini "jumping to the conclusion" ni sawa na ku"demonise" the whole process.
 
Back
Top Bottom