POTOSHI Je, hii ni hali ya mahudhurio ya wafuasi wa CHADEMA Kahama?

POTOSHI Je, hii ni hali ya mahudhurio ya wafuasi wa CHADEMA Kahama?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
1779171868100.png

1779173972854.png



​
 
Tunachokijua
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliendelea na Operesheni ya Katiba Mpya kwa Kanda ya Serengeti tarehe 18 Mei, 2026 Kahama, mkoani Shinyanga ikiongozwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho John Heche akiambatana na viongozi wengine.


Madai

Kumekuwapo na picha pamoja na video ambazo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni na kudai zikionesha hali ya mahudhurio ya wafuasi wa CHADEMA katika mkutano uliofanyika Kahama.


Uhalisia

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia marejeo ya video ya mkutano wa CHADEMA uliofanyika Kahama umebaini kuwa picha na video hizo zilirekodiwa kabla ya mkutano.

Kupitia Reverse Image search imebainika picha na video hizo zilichapishwa mtandaoni tarehe 18 Mei, 2026 kuanzia saa tisa alasiri. rejea hapa, hapa, hapa na hapa.

Kadhalika SunCalc inaonesha mji wa Kahama, Shinyanga siku ya tarehe 18, Mei 2026 mwinuko wa jua.
​
1779187711193-png.3591186

Kwenye Video: Mwanga unamulika moja kwa moja kwa juu (top-down lighting), ndio maana paa la bluu la jukwaa linang'aa lote kwa usawa na hakuna upande wa pembeni unaotupa kivuli kikubwa kuelekea uwanjani.

Hivyo video hiyo na picha zinakadiriwa kurekodiwa mchana wa jua kali, kati ya saa 6:30 mchana hadi saa 7:00 mchana muda ambao mkutano ulikuwa bado haujaanza.

Aidha saa 8 na dakika moja mchana siku hiyo ukurasa wa Chadema in blood ulichapisha video iliyoonesha kikundi cha muziki wa asili kikitoa burudani ambapo mkutano ulikuwa unaelekea kuanza.

Vilevile kupitia marejeo ya video ya mkutano huo yanaonesha idadi kubwa ya wafuasi waliohudhuria mkutano huo ukilinganisha na picha na video zinazosambazwa zikionesha wafuasi wachache.

Sanjari na hayo rejea video iliyochapishwa Instagram na John Heche ambayo pia inaonesha wafuasi wa chama hicho waliohudhuria mkutano huo.​
Back
Top Bottom