POTOSHI Je hii picha ya Rais Samia na huyu Jamaa wa Viking kufika kumpa pole Rais Samia ni halisi?

POTOSHI Je hii picha ya Rais Samia na huyu Jamaa wa Viking kufika kumpa pole Rais Samia ni halisi?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu,
Hatimaye salamu za rambirambi zimetua kutoka kwa majamaa wa viking

1789646518190.png

1789646868896.png
 
Tunachokijua
Septemba 7, 2026 Mume wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir alifariki dunia na kuzikwa siku hiyo hiyo. Baada ya tukio hilo Rais Samia amekuwa akipokea wageni mbalimbali waliofika kumpa pole.

Madai

Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo facebook kumeibuka picha inayosambaa ikiwa inamounesha Rais Samia na mwanaume mmoja aliyevalia mavazi ya asili huku akiwa na shoka na kuibua baadhi ya maswali kwamba mtu huyo aliruhusiwa vipi kuingia na silaha hiyo.

Uhalisia wa madai hayo.

Jamiicheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa picha hiyo si halisi bali imehaririwa kidigitali na kumuondoa mtu aliyekuwepo awali na kumpachika mwanaume huyo mwenye mavazi ya asili.

Kwa kutumia reverse image search imebainika kuwa picha hiyo imehaririwa kutoka kwenye picha ya halisi ambayo Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’, alifika kutoa salamu zake za pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1789647582605-png.3672531
Back
Top Bottom