SI KWELI Je, hii taarifa ni ya The Chanzo? Je, ni kweli Mapenzi ni chanzo kifo cha mtoto wa Mange

SI KWELI Je, hii taarifa ni ya The Chanzo? Je, ni kweli Mapenzi ni chanzo kifo cha mtoto wa Mange

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mange Feb 18 at.jpg
 
Tunachokijua
Mange Kimambi amejitanabaisha kama mwanaharakati wa masuala mbalimbali hususan ya kisiasa. Amekuwa akizungumzia mambo mengi ya kisiasa yanayoendelea nchini Tanzania.

Madai

Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwapo na grafiki yenye utambulisho wa The Chanzo ikiwa na ujumbe kuwa Mapenzi ni chanzo kifo mtoto wa Mange.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.

Utafututaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na The Chanzo bali grafiki hiyo ni ya kughushi kwa kutumia utambulisho wa chanzo hicho.

Picha inayoonekana kwenye grafiki hiyo na kudaiwa ni ya mtoto wa Mange ilichapshwa mtandaoni kuanzia mwaka 2024 ambapo baadhi ya vyanzo vilieleza kuwa ni mahafali ya Binti wa Mange Kimambi.

Aidha kupitia ukurasa wake wa X, Mange Kimambi hajaandika wala kuchapisha Taarifa yoyote kuhusu kufiwa na mtoto wake.

Hata hivyo kumbukumbu zilizopo zinaonesha kuwa Mange Kimambi ana watoto watatu, wa kiume wawili aliozaa na raia wa Marekani na wa kike mmoja, lakini hakuna Taarifa zinazoelezea kufariki kwa mtoto wa Mange.
1771435568840-png.3545773
Back
Top Bottom