SI KWELI Je, hii video hii ya Muafrika akitengeneza ndege ya mbao ni halisi?

SI KWELI Je, hii video hii ya Muafrika akitengeneza ndege ya mbao ni halisi?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimeona hii video na kudaiwa kuwa ni ndege ya mbao ambayo imetengenezwa na Mwafrika. Ingawa kwa upande wangu naona ni kama ina dosari zinazoonesha si halisi

Screenshot_20250902-094503_X.jpg

 
Tunachokijua
Ndege ni kifaa kilichoundwa kikiwa na uwezo wa kusafiri angani ili kurahisisha safari za masafa marefu.

Madai

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X alichapisha Taarifa inayoeleza kuwa mwanaumme mmoja wa Kiafrika ametengeneza ndege yake binafsi kwa kutumia miti, huku akiambatanisha na kipande cha video kinachomuonesha mwanaume huyo akiendelea na zoezi hilo.

Uhalisia wa video hiyo

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa video hiyo na kubaini kuwa si halisi.

Kupitia ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidigitali JamiiCheck imebaini dosari kadhaa katika video hiyo ikiwemo mwanaume anayeonekana kwenye video hiyo kutokuwa na mijengo halisi.

Matendo yanayoonekana yanakosa uhalisia, rejelea kipindi ambacho mwanaume huyo alionekana akikata kipande cha mti kwa kutumia msumeno.

Aidha ndege imekuwa ikibadilikabadilika ukubwa hivyo kukosa muendelezo wake wa muda wote katika muonekano na hivyo kudhihirisha imetengenezwa kwa teknolojia ya akili unde (AI).

JamiiCheck imetumia pia nyenzo nyingine ya kidigitali ya kubaini iwapo maudhui ni halisi ama yametengenezwa kwa Akili Unde, ijulikanayo kwa jina la Sight engine na kubaini kuwa zaidi ya 98% inaonekana kuwa ni maudhui yaliyotengenezwa kwa akili unde
screenshot-2025-09-04-081213-png.3464512
Hizi mambo zinaenda kuwa kama tishio,kuna muda huwezi tambua AI na real
 

Attachments

  • 369d74ae68f541c19e2f56c1be7d13c9.mp4
    3 MB
AI ni tishio kwa sasa..

Inaenda kufanya ushahidi wa kielectronic uwe mgumu sana kukubaliwa kuliko hapo awali
 
Ni AI hebu angalia miguu ya mzee akiwa anapanda ngazi hapo alipoweka neno "THIS IS AWESOME" kuna sehemu anakanyaga hakuna mti na anendelea kupanda tu
 
Back
Top Bottom