Zuriel_cfc
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 4,092
- 9,063
Habari za jumatatu wanajamvi.
Kuna huu utapeli unaoendelea sasa hivi mitandaoni watu kuibiwa pesa. nimeshuhudia watu watatu mpaka sasa wamelizwa hela za maana.
wakwanza ni rafiki yangu aliombwa urafiki facebook na mdada akijifanya mzungu (muingereza). wakawa wanachati mpaka wakapeana namba za wassap. huyoo "mdada mzungu" akatoa namba ya uk wakawa wanawasiliana vzr na akamwambia anatamani aje kutembea Africa na akija angependa awe mwenyeji wake. baadae mdada akamwambia rafiki yangu nataka nikutumie zawadi nipe address yako na majina kamili. rafiki yangu akatoa bila wasiwasi na huyo mzungu akamwambia ameshamtumia anaamini atazipenda.
baada ya siku tatu rafiki yangu akapigiwa simu (namba ya tz) kwamba kuna mzigo wake umetumwa kutoka Uk lakini bahati mbaya haukushushwa DSM umeshushwa Mwanza. so anatakiwa atume dola 100 ili mzigo urudishwe dar na kuna vitu vya thamani. alipouliza kuna nini akajibiwa kuna laptop, simu mbili na vikorokoro vingine. sasa huyu rafiki yangu alipomuuliza yule mzungu alichotuma akatajiwa vitu hivyo hivyo. akadata. kwa kuwa yeye ni mwanafunzi hakuwa na hiyo amount akaanza kuomba tumkopeshe, katika kumuhoji anataka hela za nini ndio kufunguka kwamba anamzigo wake katumiwa na rafiki yake kutoka Uk anataka akauchukue. watu wazima wakamwambia unaibiwa dogo. kaka yake akachukua ile namba ya tapeli akamwambia yupo pale mwanza amuelekeze ofisi alipo ili akafuate huo mzigo na ana hela mkononi. yule tapeli hakupatikana na dada akamblock rafiki yangu.
mwingine mkaka yuko zanzibar katapeliwa dolla 700 hivyo hivyo, yeye aliambiwa anatumiwa zawadi baadae akatumiwa email na mtu yupo senegal eti kapewa mzigo wake ni photocopy machine, printers na computer atume hizo dola 700 ili mzigo utumwe zanzibar. kwa kumuaminisha kwamba ametumwa na huyo mzungu, akamforwadia chati zake alizokuwa anachati (huyu mzanzibari) na huyo mzungu. jamaa akatuma hela na mzigo asipate..
mwingine huyu wa leo nae kalizwa dola 200 hapa bandarini. kadanganywa mzigo umeshukia zanzibar atume hela ili waupakie kwenye kilimanjaro matokeo yake dola zimeenda na mzigo hakuna....
hawa watu wanakuwa wahapa hapa bongo wanatumia namba za simu za nje au wanashirikiana na wa nje?
kuna yeyote imemkuta hii?
kama bado basi tahadhari kabla ya hatari.