Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Ni afadhali kuwa na nidhamu ya woga kuliko kukosa nidhamu kabisa.
Go Magufuli.
Ni afadhali kukosa nidhamu kuliko nidhamu ya woga. Nidhamu ya woga ni sawa na unafiki, lakini kwa vile watanzania wote ni wanafiki heri yako wewe ume declare kuwa bora kuwa mnafiki. Taifa la wanafiki haliendelei hata siku moja, tutapiga mark time miaka mitano.Ni afadhali kuwa na nidhamu ya woga kuliko kukosa nidhamu kabisa.
Go Magufuli.
Dah umenichekesha sana mkuu!! Kwa huyo huyu jamaa ni supervisor au manager na sio President...Wewe unaita Ze comedy lakini wataalam wa masuala ya Management watakiona kinachofanyika ni serious stuff.
Wataalam wa masuala ya management wanaita management by wandering around ambayo mwasisi wake ni Abraham Lincoln wakati wa American civil war.
Kwa msaada zaidi kama hufahamu maana ya Management by wandering around unaweza kusoma kitabu kinachoitwa, In Search of Excellence: Lessons From America's Best-Run Companies kilichoandikwa na wataalam wa masuala ya management ambao wanaitwa Tom Peters na Robert H. Waterman.
Ni afadhali kukosa nidhamu kuliko nidhamu ya woga.
ji
Hovyo kabisaNaam dadangu, aidha watu wana nidhamu au hawana. Na hakuna kitu kama "nidhamu ya woga". Ukiwa mtumishi wa umma ni lazima uogope; uogope kuvunja sheria, uogope kutumia madaraka yako vibaya, uogope kukutwa unavuruga! Unatakiwa utende kazi kwa kujiamini, kwa weledi na kwa ufanisi unaotakiwa kutokana na nafasi yako. Sasa bosi wako akitokea na kukuta umekunja nne ukaruka juu na kujimwagia chai na kuanza kujifanya unafanya kazi manake ni kuwa hukuwa mwoga in the first place! Ungekuwa unaogopa ungekuwa huna wasiwasi. Hivyo, woga wa kinidhamu unahitajika na viongozi waendelee kuwashtukiza na kuwatumbua hasa kama watumishi hawawaogopi mabosi wao au viongozi wao wajuu.
Tulidekezwa mno hadi tukadeka na kuamini tunatakiwa kudekezwa.
Hovyo kabisa
Kwani akiwa Rais anakatazwa kushughulikia mambo yaliyoko chini kabisa; au hata Katiba hamuisomi?Maajabu ya Mussa....kwa nini asingempigia katibu Mkuu au waziri badala ya kuongea na junior staff tena kwenye makamera?mawaziri wake wanajisikiaje? Hoja ya lissu ya instrument za mawaziri inapata nguvu,hoja ya lissu kwamba nchi inaongozwa na mtu mmoja kama Mali yake binafsi inapata nguvu
Braza achana na haya mambo jilindie heshima yako kidogo uliyobakia nayo kwa kukaa kimya kwa vile tunajua huwezi kumkosoa Magufuli, unafukuzia ukuu wa wilaya.Naam dadangu, aidha watu wana nidhamu au hawana. Na hakuna kitu kama "nidhamu ya woga". Ukiwa mtumishi wa umma ni lazima uogope; uogope kuvunja sheria, uogope kutumia madaraka yako vibaya, uogope kukutwa unavuruga! Unatakiwa utende kazi kwa kujiamini, kwa weledi na kwa ufanisi unaotakiwa kutokana na nafasi yako. Sasa bosi wako akitokea na kukuta umekunja nne ukaruka juu na kujimwagia chai na kuanza kujifanya unafanya kazi manake ni kuwa hukuwa mwoga in the first place! Ungekuwa unaogopa ungekuwa huna wasiwasi. Hivyo, woga wa kinidhamu unahitajika na viongozi waendelee kuwashtukiza na kuwatumbua hasa kama watumishi hawawaogopi mabosi wao au viongozi wao wajuu.
Tulidekezwa mno hadi tukadeka na kuamini tunatakiwa kudekezwa.
Soma historia ya Rais Abraham Lincoln!Ni afadhali kukosa nidhamu kuliko nidhamu ya woga. Nidhamu ya woga ni sawa na unafiki, lakini kwa vile watanzania wote ni wanafiki heri yako wewe ume declare kuwa bora kuwa mnafiki. Taifa la wanafiki haliendelei hata siku moja, tutapiga mark time miaka mitano.
Mfano siku ile Wilson Kabwe anatumbuliwa nikajua mikataba yote ya makusanyo ya mapato kwenye vyanzo vikuu kama stendi na masoko ya nchi nzima vitaangaliwa na kuwatumbua wengine. Cha ajabu utumbuaji uliishia pale kwa vile ulimlenga mtu na sio mfumo.
Ili kumsaidia raisi wetu tumpatie ushauri mzuri, yeye ni mkubwa sana kuhojiana na mkaguzi wa airport, angeangalia kazi inafanyikaje anaenda kujadiliana na waziri wake na mkuu wa airport anaelezwa procedure na kushauri njia bora. Yaani tuanze tena kukaguliwa mizigo yetu tukifika tunakoenda kwa ajili ya kumfurahisha mtu mmoja JPM. Ama kweli upele umepata mkunaji
Ukikosa nidhamu unafukuzwa kazi anawekwa mtu mwingine mwenye nidhamu kazi inaenda. Ni kitu rahisi, nidhamu ya woga ni yule nesi anayenyenyekea wakati yuko na boss wake halafu boss akiondoka anapiga vibao wajawazito. Hatutaki nchi ya namna hii, tunataka nchi ya watu wenye nidhamu ya kumwambia Magufuli kuwa hata ukienda JFK airport mizigo ya arrivals haipiti kwenye ukaguzi tena kwa vile ilikaguliwa ilikopita unless iwe imetiliwa mashaka. Na jibu la namna hiyo anatoa mkurugenzi wa shirika au taasisi husika na sio ATTENDANT kama yule aliyekuwa anahojiwa na JPM. Mtu mwingine anaweza kuwa na furaha isiyo na kifani kukutana uso kwa uso na mkuu wa nchi akajibu maswali kwa ufasaha na mwingine anaweza kutetemeka akashindwa kuongea au akaongea kumfurahisha mkuu. Suluhisho ni raisi kupita na kuangalia systems and procedures akikuta kuna shida anawaita wahusika anatumbua au anaunda timu ya uchunguziKwa hiyo ni afadhali ukose huduma hospitalini (mfano) kwa sababu kuna mkubwa mmoja ameamua kuuza dawa kwa kuwa haogopi?
Naijua historia ya Abraham Lincoln na sijaona popote alipozunguka marekani nzima kukagua kazi. Lincoln anasifika leo hii Marekani nzima kwa vile aliweka mifumo na misingi imara ambayo ilipelekea hadi kufanyika THE SECOND AMENDMENT ambayo Leo hii baadaye sana watu wa Marekani wanafaidi matunda. Kila sehemu kuna systems, procedures na regulator. Mfano mzuri wana vyombo kama NTSB, hata ukiingizi guta lako barabarani likaua watu hawasubiri Obama atoe amri, kesho yake watu wanaingia kaziniSoma historia ya Abraham Lincoln!
Nimetoa mfano wa Abraham Lincoln kwa sababu wakati anafanya management by wondering alikuwa ni Rais.
Kikubwa kabisa, Kwani anachokifanya Rais Magufuli ni nje ya mipaka yake ya kazi? Au mnajaribu kumpangia mipaka ya kazi nje ya Katiba ya Tanzania.
Hujaona Rais Abraham Lincoln anazunguka wapi wakati nimekupa aina ya utendaji wake wa kazi ambao mpaka leo Taifa la Marekani linamkumbuka.Naijua historia ya Abraham Lincoln na sijaona popote alipozunguka marekani nzima kukagua kazi. Lincoln anasifika leo hii Marekani nzima kwa vile aliweka mifumo na misingi imara ambayo ilipelekea hadi kufanyika THE SECOND AMENDMENT ambayo Leo hii baadaye sana watu wa Marekani wanafaidi matunda. Kila sehemu kuna systems, procedures na regulator. Mfano mzuri wana vyombo kama NTSB, hata ukiingizi guta lako barabarani likaua watu hawasubiri Obama atoe amri, kesho yake watu wanaingia kazini
Nimesema hovyo kabisa..sio hovyo tuHaitoshi kusema "hovyo" ukafikiria umesema kitu chenye akili; onesha uhovyo wenyewe ili angalau tuone kuwa umetumia chembe za ubongo vizuri...
Kama umenielewa nimesema nataka raisi Magufuli aweke misingi ambayo hata akikaa ofisini au yuko nyumbani na mama yetu Janet, huku chini kila mtu anatimiza wajibu. Asiye timiza wajibu na mwenye nidhamu ya woga anatumbuliwa huko huko na mkubwa wake. Hii itamsaidia sana raisi na misingi hii iko kwenye katiba ya WariobaHujaona Rais Abraham Lincoln anazunguka wapi wakati nimekupa aina ya utendaji wake wa kazi ambao mpaka leo Taifa la Marekani linamkumbuka.
Tatizo lenu mnataka Tanzania ya leo iwe kama Marekani ya leo bila kufahamu kuwa hata Marekani ya 1860 ilikuwa kama Tanzania ya leo ndiyo maana watu kama Rais Abraham Lincoln wakaja na aina ya utawala ambao ulijenga misingi ambayo umeifanya Marekani kuwa Taifa lenye nguvu kiuchumi na kisiasa.
Sisi tunataka Rais Magufuli afanye kama anavyofanya Rais Obama wakati taasisi zetu ni kama za Marekani ya miaka ya 1860 iliyokuwa chini ya Rais Abraham Lincoln.