Je hizi tetesi kuhusu Abdi banda kujitoa Timu ya taifa ni kweli

Je hizi tetesi kuhusu Abdi banda kujitoa Timu ya taifa ni kweli

Kalolelo

Senior Member
Joined
Oct 17, 2018
Posts
164
Reaction score
244
Beki wa kimataifa wa Tanzania anaecheza soka la kulipwa nchini Africa Kusini kwenye klabu ya baroka Fc inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama ABSA PREMIER LEAGUE.
ABDI HASSAN BANDA amejitoa timu ya taifa mpaka muda wa Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania mnigeria Emmanuel Amunike utakapomalizika.

Hayo yametokana na Mara baada ya kutoa ushauri kabla ya mchezo wa Lesotho kwa kumwambia awatoe mabeki katika nafasi za mawinga na kuwaweka nafasi zao wanazochezaga. Kocha Huyo alikataa na kumtoa nje ambapo beki huyo kisiki alikabidhi jezi yake kwa wachezaji wenzake na kuwaambia hachezi tena national team mpaka muda wa Kocha huyo utapomalizika na kuamua kupanda jukwaani kukaa na mashabiki kuangalia mtanange huo ambapo Tanzania ilipoteza kwa kukubali kipigo cha goli moja kwa sifuri.**
 
Tayari kuna taarifa zinazagaa mitandaoni kuwa Banda amekanusha!

Kimsingi mpk leo najiuliza na humu nimeuliza, watu wote waliokuwa na timu Lesotho, including Hemed Morocco - Assistant Coach pamoja na Danny Msangi - Team Manager! Hakuna aliepata uthubutu wa kumwambia Amunike km anakosea kuwapeleka wings wawe full backs ilhal wingi by nature walikuwepo?

Zayd ni natural wing! Msuva ni natural wing! Shiza ni natural wing! Ulimwengu!
 
Atoke tuu,maana ameshakuwa Kama Ali kiba kazi vijembe tu vya kumsupport shemeji yake mitandaoni badala ya kucheza mpira
 
Beki wa kimataifa wa Tanzania anaecheza soka la kulipwa nchini Africa Kusini kwenye klabu ya baroka Fc inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama ABSA PREMIER LEAGUE.
ABDI HASSAN BANDA amejitoa timu ya taifa mpaka muda wa Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania mnigeria Emmanuel Amunike utakapomalizika.

Hayo yametokana na Mara baada ya kutoa ushauri kabla ya mchezo wa Lesotho kwa kumwambia awatoe mabeki katika nafasi za mawinga na kuwaweka nafasi zao wanazochezaga. Kocha Huyo alikataa na kumtoa nje ambapo beki huyo kisiki alikabidhi jezi yake kwa wachezaji wenzake na kuwaambia hachezi tena national team mpaka muda wa Kocha huyo utapomalizika na kuamua kupanda jukwaani kukaa na mashabiki kuangalia mtanange huo ambapo Tanzania ilipoteza kwa kukubali kipigo cha goli moja kwa sifuri.**

Ni kweli Kocha wa Taifa Stars anaweza kuwa na ' mapungufu ' yako ila niseme tu ukweli wangu kwani sijazoea ' Unafiki ' kwamba ifike muda sasa Abdi Banda a.k.a Binyo abadilike kwani nidhamu yake hasa akiwa huku Tanzania huwa inakuwa mbaya. Ana dharau sana, maringo ya Kishamba na anaona ameshafika tayari Premier League au La Liga kumbe bado yupo tu hapo PSL ya Afrika Kusini.

Huwa kila mara najiuliza hivi leo hii Banda angekuwa na mafanikio aliyonayo Mbwana Samatta a.k.a Poppa akina Sisi tungekunywa hata Maji? Abadilike kwani bado hajachelewa na ana Kipaji kizuri na kikubwa mno.
 
Akijitoa Sawa ashajiona hawezi

Ova
Yaani tatizo letu ni kuona kuchezea timu za Yanga na Simba ndo mwisho wa dunia ya soka. Huyu kwenda Sauzi kaona anamzidi Amunike, aibu mno. Amunike ni mchezaji wa kimataifa licha ya ligi huko Ulaya kombe la dunia kwa timu yake kachezea mara nyingi tu.
 
Tusipende kuhukumu mapema jamani dunia ya sasa ya mitandao imejaa uzushi sana..jamaa amekanusha
Screenshot_2018-11-23-21-26-51-1.jpg
 
Huyu kocha si aende akawafundishe Boko Haramu jinsi ya ku play fair
 
Back
Top Bottom