Je, hoja za Nyalandu zimejibiwa?

Je, hoja za Nyalandu zimejibiwa?

Haya mambo yangetokea wakati Magu akiwa hai (akiwa kamaliza muda wake wa Rais,akamwachia mwingine,,naamini asingekuwa mwanamama)... Nadhani Familia ya JPM inateseka kwa yanayotokea
Angekuwa Kakuru,, ndo maana akina Mjaliwa na Kubudi walianza kupanguliwa mapema,, waliambiwa ni wazee hawawezi kuwa marais.[emoji3][emoji3]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nyarandu dingi bishoo anapenda show off anajua akiwa sisiemu atapata kamseleleko. Hana jipya ni snitch ka wengine.
 
MTU mpenda haki asiye muoga,mshika mawaidha ya dini asiye na tamaa,msimamia ukweli asiyefata upepo asingeweza kuhudumu kwenye serikali ya awamu ya tano!! Kulijawa ubabe,uvunjifu wa katiba na sheria,visasi na visa, ubaguzi na ukandamizaji na mengi yasiyofaa kwa msukumo wa mtu. Ilikuwa sawa Nyalandu kujiuzulu na kama MTU hayupo tena nisawa akirudi!! Membe naye arudi kwa wazee wenzake sasa
 
JE, HOJA ZA MHE NYALANDU ZIMEJIBIWA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo Mhe Nyalandu aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amerudi CCM katika Mkutano mkuu maalum uliofanyika hapa Jakaya Kikwete Convention. Mhe Nyalandu anarudi CCM baada ya kujivua uwanachama wa CCM tarehe 30/10/2017.

Kama ilivyo kwa watu wengine wanapohama Chama kimoja kwenda kingine huwa wanakuwa na sababu lukuki zinazowafanya kuhama vyama vyao. Ndugai naye akiwa anaondoka na kujivua ukada wa CCM alielekeza shutuma kuwa Katiba ya nchi si rafiki. Alisema kuwa mihimili haijitegemei.

Maswali ya kujiuliza ni kuwa Mhe Nyalandu hoja zake alizokuwa akizisimamia zimefanyiwa kazi? Je, Nyalandu aliukimbia utawala wa hayati Magufuli au aliikimbia Katiba? Kama ni Katiba mbona bado ni ile ile aliyoikimbia? Je, Mhe Nyalandu anaamini katika utawala au katika Katiba?

Mhe Nyalandu, aliyewahi kuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii wakati wa serikali ya awamu ya Tano wakati anatimukia CHADEMA alisema kupitia taarifa yake kwamba amejuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama cha mapinduzi CCM ikiwemo ubunge wake.

Nyalandu alisema amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa na mwendo wa siasa nchini Tanzania, ukiukwaji wa haki za kibinaadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu dhidi ya raia na kutokuwepo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola - Serikali, Bunge na Mahakama. Hizi zilikuwa ni tuhuma kubwa kutokea kutoka kwa mtu aliyekuwa ndani ya serikali ukimuondoa mzee Mrema.

Katika taarifa yake ya kujiuzulu aliyoiweka katika ukurasa wake wa Facebook ambayo hadi muda huu ninaandika hakuifuta, Nyalandu alisisitiza umuhimu wa nchi kupata katiba mpya.

Mhe Nyalandu alisema "Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali,"

Kwa hoja hizi za kuondoka kwa Mhe Nyalandu na kurudi tena leo CCM ingali bado hoja yake ya Katiba mpya haipo, Basi inaonyesha namna Wanasiasa wengi tulivyo na ndimi mbili. Inaonyesha namna Wanasiasa tunavyotumia fursa za Siasa vibaya. Nyalandu sasa anaowajibu wa kuwaeleza Watanzania kuwa sababu iliyomkimbiza CCM haikuwa Katibu mpya kwa mwamvuri wa Mhimili kuto kuwa independent bali alikuwa na sababu nyingine.

Ni vema kama Taifa tukajenga siasa za ushindani bila uzushi na kutengenezeana ajali.
Wanasiasa vwatakuumiza kichwa brother focus kwenye issue zako
 
Back
Top Bottom