Je huu mkakati wa kusambaza mitungi ya gas ya LPG sio mpango wa kuhujumu matumizi ya gas ya NPG inayopatikana Tanzania?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Wafanyabiashara wenye kuagiza bidhaa muhimu toka nje tumeona kila wakati wakihujumu mipango ya taifa ya kuzalisha bidhaa hizo nchini. Tumeona kwa mfano wakihujumu uzalishaji wa ngano ili biashara yao na wabia wa nje isife. Tumeona mfano huo kwa uzalishaji wa sukari kila wakati kukiwa na hujuma hadi sukari inaagizwa nje huku viwanda vipo na mahitaji ni makubwa.
Tunajua jitihada huko nyuma kutengeza vipuri vya magari na mashine wakati wa awamu ya mwalimu nyerere zikihujumiwa na waagizsji wa vipuri.
Kuhusu hili la kusambaza mitungi ya gas ya LPG na gas yenyewe kona zote za nchi ili kulinda mazingira ni jambo zuri. Ila binafsi sijui kama lengo la kutumia gas inayozalishwa nchini ambayo ni gas asili NPG limezingatiwa. Kwamba nchi itakapokua tayari kusambaza gas yake kwa matumizi ya nyumbani mitungi wanayosambaziwa wananchi vijijini kwa sasa itaweza kutumika. Tunajua mitungi tu inaweza kua kikwazo kwa wananchi vijijini kutumia gas asilia ambayo tumaini la wananchi ni lazima iwe na bei nafuu kuliko gas inayoagizwa kutoka nje.
Tunaojua hila na mbinu za wafanyabiashara tuna shaka zoezi la kusambaza mitungi ikawa pamoja na kuokoa mazingira lkawa hujuma kwenye usambazaji wa gas inayopatikana nchini. Makampuni yanayouza gas za nje bila shaka yana mpango madhubuti kulinda biashara zao.
 
Kuna tofauti gan kati ya NPG na LPG?
 
LPG (Liquified Petroleum Gas) ni gesi ya petroli iliyochomwa na kuhifadhiwa kama kioevu. Huku gesi asilia ni gesi ambayo hutokea kwa asili na kwa kawaida huhifadhiwa na kusafirishwa kama gesi.

Tofauti kuu:
  • Chanzo: LPG hutokana na mafuta ghafi, wakati gesi asilia hutokea kwa asili.
  • Utendaji: LPG huwaka haraka na kwa joto kali zaidi kuliko gesi asilia.
  • Bei: LPG kwa kawaida ni ghali zaidi kuliko gesi asilia.
  • Usalama: LPG ni hatari zaidi kuliko gesi asilia kwa sababu huwaka kwa urahisi zaidi.
Kuna tofauti gan kati ya NPG na LPG?
 
Au basi tuachane na yote. Kila familia au kijimtaa wajizalishie Methane yao watumie. Matakataka ozo yapo mengi tu na vinyesi zipo za kutosha.

Kwa nini tusishadadie methane badala ya kuhangaishana ooo mchango wa taka sasa taka iwe mali
 
Kuna tofauti gan kati ya NPG na LPG?
LPG ni kifupi cha liquified petroleum gas. Hii ni gesi inayozalishwa wakati wa kuchuja crude oil kwenye refineries kupata petrol, diesel, mafuta ya taa etc. Kwenye hii process ndio pia unapata gesi ya LPG. Hapa nchini kama ilivyo mafuta ya petroli tunaagiza kutoka nje.
NPG ni natural petroleum gas. Hii inapatikana moja kwa moja toka ardhini. Ndio gesi kama hii yetu insyopatikana Mtwara na kusafirishwa kwa bomba hadi dar kuzalisha umeme na pia kusambazwa kwa baadhi ya nyumba kwa matumizi ya nyumbani.
 
ufafanuzi mzuri.
 
Gasi asili haiko kwenye kumiminika rahisi Kwa Ajili ya matumizi kama hiyo nyingine.

Hakuna hiyo Huduma ,by the way Serikali Iko kwenye majadiliano na Uganda,Kenya na Zambia Ili kujenga mabomba ya kwenda Nchi hizo kuuza gesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…