kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Wafanyabiashara wenye kuagiza bidhaa muhimu toka nje tumeona kila wakati wakihujumu mipango ya taifa ya kuzalisha bidhaa hizo nchini. Tumeona kwa mfano wakihujumu uzalishaji wa ngano ili biashara yao na wabia wa nje isife. Tumeona mfano huo kwa uzalishaji wa sukari kila wakati kukiwa na hujuma hadi sukari inaagizwa nje huku viwanda vipo na mahitaji ni makubwa.
Tunajua jitihada huko nyuma kutengeza vipuri vya magari na mashine wakati wa awamu ya mwalimu nyerere zikihujumiwa na waagizsji wa vipuri.
Kuhusu hili la kusambaza mitungi ya gas ya LPG na gas yenyewe kona zote za nchi ili kulinda mazingira ni jambo zuri. Ila binafsi sijui kama lengo la kutumia gas inayozalishwa nchini ambayo ni gas asili NPG limezingatiwa. Kwamba nchi itakapokua tayari kusambaza gas yake kwa matumizi ya nyumbani mitungi wanayosambaziwa wananchi vijijini kwa sasa itaweza kutumika. Tunajua mitungi tu inaweza kua kikwazo kwa wananchi vijijini kutumia gas asilia ambayo tumaini la wananchi ni lazima iwe na bei nafuu kuliko gas inayoagizwa kutoka nje.
Tunaojua hila na mbinu za wafanyabiashara tuna shaka zoezi la kusambaza mitungi ikawa pamoja na kuokoa mazingira lkawa hujuma kwenye usambazaji wa gas inayopatikana nchini. Makampuni yanayouza gas za nje bila shaka yana mpango madhubuti kulinda biashara zao.