Je, huu ni mchezo mchafu?

Je, huu ni mchezo mchafu?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kuna ndugu yangu mmoja ana account huko CRDB, ila anasema haijatimia kwa muda mrefu kidogo.
Sasa wiki ya pili anapokea jumbe za alerts kuwa account yake imepokea sh. Kadhaa, mara baada ya muda mfupi anapokea tena jumbe kuwa account yake imetolewa fedha kiasi kadhaa sawia na ile pesa iliyoingia.
Nilimwambia aangalie Salio akasema kadi hajui iko wapi na app haiko kwenye simu yake. Alihisi account kapewa mtu mwingine.
Nikamwambia watu wa benki wako makini sana hawawezi kumpa mtu account yenye usawia na ya mtu mwingine. Pia kwanini namba ya simu hawajabadili.
Mimi nimemsanua may be ni mapapa, na asipoangalia jela inamngoja maana ni pesa nyingi sana.
Milioni mia , mia na kitu, milioni tisini, milioni mia mbili n.k
Kama ni mchezo mchafu nani anaibiwa?
Pesa wanasema zimetoka kwa swift
 
Hahaha ukiona mtu anaogopa pesa, jua ni za mgao wa wale WASIOJULIKANA.

Deals zao huwa wanapeana cash, ukiona mtu ana account inasoma miliini 200, mara wametoa mil 100 hashtuki, usimuone mjinga, anajua ni HONEY TRAP.

Mitego hiyo sogea udakwe, nenda wewe ukaseme ni zako uozee jela.

Ukiwa attached na pesa, wanawake au familia usiwe jambazi au usifanye deals chafu, utakamatwa kama panzi.

KAMA HAZIMSHITUI MUHUSIKA, HATA WEWE USIZITAMANI.
 
Kuna michezo huwa inafanyika kwa kudhirikiana na wafanyakazi wa benki
Wao wanatoa siri za account ambazo ziko dormant kwa muda mrefu halafu zinatumika kupitisha pesa za dili
Eeeh kumbe? Kuna siku nilipokea ujumbe toka benki, account yangu imehusika na malipo ya kampuni ya mafuta( moja kati ya makampuni makubwa ya mafuta yenye matank kule kigamboni). Nikapuuza kwa kuwa ni account ambayo sikuweka pesa muda.
Mara ya pili nikapata ujumbe mwingine, nikapuuza pia kwa kujua wanakosea.
 
kuna bodaboda mmoja alikuwa anatumia simu mbovu kitochi kinazima zima, nampigia simu aje anifate nipo car wash naacha chuma inapigwa maji simpati kwenye simu,

nikaona isiwe tabu nikaingia barabarani natembea kuelekea kituo cha boda jirani nikamkuta huyo boda nliekuwa nampigia amekaa tu, nikamuambia unakaa tu hupatikani unakosa hela wewe.

Akaangalia simu imezima ile kuiwasha zikaingia sms mbili imethibitishwa umepokea laki8 na nyingine muamala umezuiewa pesa zimerudishwa,

Huyo Boda alijilaumu sana kesho yake nilimuagiza apeleke mazaga home ananambia usiku hata hakulala ile hela ilikiwa inamuuma sana.
 
Kuna ndugu yangu mmoja ana account huko CRDB, ila anasema haijatimia kwa muda mrefu kidogo.
Sasa wiki ya pili anapokea jumbe za alerts kuwa account yake imepokea sh. Kadhaa, mara baada ya muda mfupi anapokea tena jumbe kuwa account yake imetolewa fedha kiasi kadhaa sawia na ile pesa iliyoingia.
Nilimwambia aangalie Salio akasema kadi hajui iko wapi na app haiko kwenye simu yake. Alihisi account kapewa mtu mwingine.
Nikamwambia watu wa benki wako makini sana hawawezi kumpa mtu account yenye usawia na ya mtu mwingine. Pia kwanini namba ya simu hawajabadili.
Mimi nimemsanua may be ni mapapa, na asipoangalia jela inamngoja maana ni pesa nyingi sana.
Milioni mia , mia na kitu, milioni tisini, milioni mia mbili n.k
Kama ni mchezo mchafu nani anaibiwa?
Pesa wanasema zimetoka kwa swift
project managers wa mabenk mara nyingi huwa wanatumia izo account kufanyia majaribio ya project zao
 
Kuna michezo huwa inafanyika kwa kudhirikiana na wafanyakazi wa benki
Wao wanatoa siri za account ambazo ziko dormant kwa muda mrefu halafu zinatumika kupitisha pesa za dili
Naunga mkono hii hoja yako! Siku Moja nilienda kufanya mchakato wa mkopo baada ya mkopo kutoka Kuna kiasi ambacho walikikata sikuelewa kwa nini wanakata ila Wakasema hiyo pesa inayokatea utarudishiwa baada ya miezi 3! Hii kitu ilinipa maswali mengi sana lakini wakaniambia niondie wasiwasi hyo pesa utaipata nikachukulia poa TU!

Sasa kwenye kuipata nilimpigia simu nyingi sana na mizungusho isiyo ya maana lakini baadae wakaniwekea baada ya kumwambia mitamuona meneja!

Awamu nyingine hapo ndipo nilipata hisia Fulani ya kua Hawa jamaa Huwa wanatumia mkopo wako kujikopesha!

Awamu ya pili nilipoenda kuchukua mkopo afisa Moja aliyenifanyia mchakato alikua mshikaji hvyo lakini pesa ilivyoingia akaja jamaa mwingine akaniambia utakatwa kiasi kafulani ambacho utakipata baada ya miezi 3!
Daah nikaona hapa nataka kupigwa nikamfuta mshikaji akaniambia usiwe na wasi hyo pesa utaipata! Nikaona poa nikasepa muda ulipofika jamaa nikamcheki akaniambia Sasa pesa yako utaingiziwa Leo lakini itaingia kiasi Fulani zaidi ya kile kiasi na akaniambia hichokiasi kilichozidi utakata kiasi Fulani alafu utanitumia kwenye Simu.

Hapa nikagundua kua Hawa jamaa itakua wanajikopesha kupitia mkopo wa mteja na usipoidai hyo pesa ndiyo inakua mazima!
Na Hilo swala la kupokea jumbe za kupokea pesa na kutolewa limeshanikuta sana baada ya akaunti yangu kutotumika kwa muda mrefu!
 
Back
Top Bottom