Je, huu ni mwendelezo wa Serikali kutudharau Walimu Shule za Msingi?

Je, huu ni mwendelezo wa Serikali kutudharau Walimu Shule za Msingi?

Weakman

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2021
Posts
995
Reaction score
1,607
Nipo shuleni ofisini

Mbele yangu Kuna mzigo mkubwa wa daftari za stadi za kazi darasa la tano ninazopaswa kusahisha

Naangalia nje namuona mwalimu wa sekondari yuko bize kusimamia mtihani wa darasa la Saba

Najiuliza kwanini nisisimamie mwenyewe mwalimu wa shule ya msingi?

Je, Serikali imenichukia sana kiasi cha kuninyang'anya majukumu yangu?

Hili limenisikitisha sana nahisi nakosa furaha yangu ya kawaida hapa shuleni

Ni kawaida yangu asubuhi kuwatia moyo watahiniwa kuwa watulivu kisaikolojia ila ukweli leo nimejikuta nimeshindwa kufanya hivyo

Je, huu ni muendelezo wa serikali yetu kutudharau waalimu shule za msingi?
 
Kwa kuwa nyie ni sehemu muhimu kwenye zile chafuzi kuu na chafuzi za mitaa wote kwa umoja wenu mnastahili kulipia madhambi yenu kwa raia wote wataifa hili wanaopenda haki na kuchukia uonevu ambao nanyi ni sehemu yake.
 
Weakman pole sana, serikali ya CCM haiwajali watumishi hasa walimu ambao kila siku wanaibakura na kuwaweka madarakani kwa sababu miaka yote walimu wamekuwa wakisaidia kuiba masanduku ya kura wakisaidiana na genge la polisi,miaka ya hivi karibuni kulitokea mtindo wa wanaccm kuwaambia kuwa walimu wakuu wanaofelisha wataondolewa kwenye vituo vyao kwa kupunguzwa madaraka!

Sasa baada ya hao wanasiasa katili kuvamia Elimu kwa kutaka sifa walimu wakuu wakaanza kuiba mitihani na kuwafanyia wanafunzi wao matokeo yake kuna miaka kama ishirini hapa nyuma watoto wetu wanapelekwa sekondari huku hawajui kusoma na kuandika huku wanaccm wakipata sifa kwamba ufaulu umekuwa mkubwa kwa kuwahadaa wananchi kwamba serikali inafanya vizuri kumbe ni changa la macho na wananchi wa Tanzania walivyokuwa wajinga hawaulizi wamekaa kimya huku watoto wao wakipotea kwa uzembe wa serikali hali hiyo imeendelea kwa miaka yote hadi hivi leo,

Sasa mwaka 2015 ile hadaa ya Magufuli kwamba tuanze elimu bure ikapamba moto huku wanafunzi 1212900 wakiandikishwa darasa la kwanza CCM wamekuja kutaamaki mwaka huu mwezi January kwamba tunatakiwa kujenga vyumba vingi vya madarasa huku pesa ya kujengea haipo kwa nchi nzima, mwaka huu ili kupunguza hizo alama za ufaulu wameamua kuwapeleka watu ambao hawanataaluma za kusimamia mitihani lengo likiwa ni kupunguza alama baada ya kuona walimu watawafanyia wanafunzi mithani na kufaulisha kwa alama nyingi hivyo wameamua kuwaondoa kupitia watumishi wengine maana kwa idadi ya wanafunzi huku CCM hawana uwezo wa kujenga madarasa na mwisho niseme tu SAMIA NI DICTATOR WA KIKE ASANTE
 
@Weakman pole sana, serikali ya CCM haiwajali watumishi hasa walimu ambao kila siku wanaibakura na kuwaweka madarakani kwa sababu miaka yote walimu wamekuwa wakisaidia kuiba masanduku ya kura wakisaidiana na genge la polisi,miaka ya hivi karibuni kulitokea mtindo wa wanaccm kuwaambia kuwa walimu wakuu wanaofelisha wataondolewa kwenye vituo vyao kwa kupunguzwa madaraka...
Sina neno la kusema,napita tu.
 
Mleta mada kama ni mwalimu serikali ilikuajiri kimakosa

Hiyo kitu inaitwa segregation of duties

Huwezi kufundisha wewe,utunge mtihani wewe,usimamie wewe na usahihishe wewe!!!
Basi kama nawe ni mwimba mapambio uliajiriwa ilivyostahili.
 
Walimu wa msingi mlikuwa na kasumba ya kuiba mitihani na kuisovu kisha mnawapa wanafunzi vimemo vya majibu wanaingia navyo kwenye chumba cha mtihani.

Matokeo yake mkatuzalishia wanafunzi ambao hawajui kusoma wala kuandika kujiunga sekondari. Naona mwaka huu serikali imewabana sasa mmeanza kutoa milio ya kila aina. Hahahhahahah Tulieni dawa iwaingie
 
Walimu wa msingi mlikuwa na kasumba ya kuiba mitihani na kuisovu kisha mnawapa wanafunzi vimemo vya majibu wanaingia navyo kwenye chumba cha mtihani. Matokeo yake mkatuzalishia wanafunzi ambao hawajui kusoma wala kuandika kujiunga sekondari. Naona mwaka huu serikali imewabana sasa mmeanza kutoa milio ya kila aina. Hahahhahahah Tulieni dawa iwaingie
Umesahau sekondari walikuwa wanasovu mitihani kidato Cha 4, serikali ikaamua kupeleka ulinzi wa polisi

Wakahamia kusovu mitihani kidato Cha 2 na serikali ikapeleka ulinzi wa polisi

Sasa unashangaa walimu msingi?

Serikali ilinde mitihani, sio kutunyang'anya mitihani yetu
 
Walimu wa msingi mlikuwa na kasumba ya kuiba mitihani na kuisovu kisha mnawapa wanafunzi vimemo vya majibu wanaingia navyo kwenye chumba cha mtihani. Matokeo yake mkatuzalishia wanafunzi ambao hawajui kusoma wala kuandika kujiunga sekondari. Naona mwaka huu serikali imewabana sasa mmeanza kutoa milio ya kila aina. Hahahhahahah Tulieni dawa iwaingie
Nyie pambaneni na hali yenu, akiwemo pamoja na Yehodava kwani nae ni mmoja wenu.
 
Hiyo miaka ya mwanzo hawakuliona hilo?

Na je hiyo mitihani ya form 4 na 6 wataenda kusimamia walimu wa msingi?
Kwa swali hili na logic uliyoitumua hapa kweli wewe ni Mwalimu.

By the way hii kazi ilikuwa wito wewe furaha yako ni kufundisha na kuelimisha na sio kupata sifa au ujira, kwahio kama vile akunyimae Kunde anakupunguzia Mashuzi, vilevile aliyekunyima kusimamia basi amekuongezea muda wa kusahihisha na kuwanoa wanafunzi wako.
 
Mleta mada kama ni mwalimu serikali ilikuajiri kimakosa

Hiyo kitu inaitwa segregation of duties

Huwezi kufundisha wewe,utunge mtihani wewe,usimamie wewe na usahihishe wewe!!!
Kule chuo kikuu unakojinadi ulisoma mitihani ya kozi Yako ilitungwa na kusahihishwa na necta? Au ilitungwa na kusahihishwa chuo tofauti na ulichosoma? Usidanganye kiitikadi!
 
Katunga mtihani lini?
Mitihani ya shule za msingi hutungwa na walimu wenyewe wa shule za msingi! Siyo lazima awe mtoa mada. Na sekondari nako ni hivyo hivyo. Baraza la Mitihani laTaifa (NECTA) ni wasimamizi tu. Ila kila kitu kinacho husiana na mitihani, hufanywa na walimu wenyewe.

Safari hii Baraza limeamua kufanya hivyo kama majaribio baada ya kugundua tatizo la udanganyifu limeendelea kuwa changamoto kwa mtihani wa darasa la saba ukilinganisha na mitihani mingine.

Na huenda wamegundua baadhi ya walimu wa shule hizo, ni wanyonge kwa wakubwa zao wanao walazimisha kushiriki kwenye huo udanganyifu! Thats why wakaamua kuwachukua walimu wachache wa sekondari na kuwa wasimamizi wakuu wa mitihani ya mwaka huu.

Hivyo walimu wa primary wanatakiwa kujifunza kitu kutokana na kuachwa baadhi yao kusimamia hii mitihani.
 
Pole Sana mwalimu, tatizo wengi wenu walikua washajiwekea ulaji, ukienda kusimamia unapewa lak 3 had 5 af pepa ikianza mnachukua pepa moja kusolve na kurudisha majibu kwa watoto. Matokeo yake secondary wanaenda vilaza hawajui kusoma Wala kuandika.

Mwaka huu mmepatia dawa, ni matokeo ya kupoteza uaminifu. Na asilimia kubwa ya walimu waliokuja kusimamia hua wanafanya kazi za Baraza zenye hela kuliko hizo laki 5 hivyo hawahongeki kirahisi wasije kupoteza nafas zao. Acheni wafaulu wenye sifa.

Kusema na nyie msimamie secondary hakuna mashiko. Kwanza Secondary hakuna udanganyifu uliokithiri Kama msingi na hata ungekuwepo huwezi kuthibitiwa na wadanganyifu walewake wa msingi, pili asilimia kubwa ya walimu msingi hawajafika form six hivyo hawana hata experience ya mtihani wa six mfano hawez jua Majukumu ya mwl wa practical kwenye chumba Cha mtihani nk.

Pole Sana mwalimu Ila Hongera pia, kuanzia Sasa ukikosa nafasi hiyo usijutie hata sio dili Kama zamani. Unaepushwa na mengi haya mabadiliko sio kwa wasimamizi tu unaweza kujikuta umeingia matatizoni na hata umepoteza ajira yako au kuwekwa ndani.
 
Back
Top Bottom