Je huu ni uchawi wa namna gani?


kaka pole sana, kama story yako ni ya kweli nakushauri uhame fasta maana atarudi kukufanyizia zaidi ya hayo yote uliyomtendea. tena hama haraka acha masikhara huyo kwako ni adui tayari.
 
Uchawi kusema kweli upo, tena ni mwingi balaa. Anayebisha afike hapa temeke hospital aone picha za wale watu waliong'ang'aniana wakati wakibanduana kinyume na maumbile.
 
kuna jamaa ni mwizi wa pikipiki tabata
juzijuzi alipigwa vibaya mno hakutoa damu hata tone kuna jamaa akachukua panga buchani wakamlaza akalipiga kwenye shingo likadunda tu halikumkata ,yaani kila mtu alishangaaa.

kuna mzee akasemalile panga lingepigwa kwanza chini
kuna maajabu kweli dunia hii.
 
haya mambo yapo nimeshuhudia kesi kama hizo kwa macho yangu mwenyewe kama mara 2, na kuhadithiwa mara nyingi tuu. Kunammoja hapa shule ya uhuru ikiwa stand ya Goms kabla ha kujengwa Benjamin mkapa kunakibaka alishikwa, watu piga sana lakini jamaa anaonekana yupo ngangali.

Watu wakaiona iridhi yake kwapani , ilipokatwa tu jamaa akaanza kuishiwa nguvu na akalakichapo ashukuru mungu polisi walimwokoa.
 
Duuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!! ni balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Nilitaka kusema hilo. Jamaa wangemmulika na tochi halafu wakishughulikie kivuli. Vibaka wa aina hii tulishakuwa nao wengi sana huko kwetu na wote tuliwamaliza kwa style ya kuangamiza kivuli.
 
ni mwizi na amejikinga na dawa za kienyeji hizo za kiganga, ndio kawaida ya wezi waliokomaa wengi hujikinga. labda pi sio binadamu ni jini fulani au linyama linajigeuza kuwa mtu.

msingemuachia mngeanza kusali hapo labda angewaabia mengi zaidi. ila mna roho mbaya haswa wewe kwanini hukuita polisi au kumpeleka huko?

unataka kuua kisha gari, then uachiwe laana za kukufata jneration yako yote, duh
 
Duh! Wazee uchawi noma kitaa che2kuna mzee anapiga miselena paka wa kutosha ukimzingu ucku hulali.
 
Tutumie picha tuamini

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Uchawi wa kihivyo sijawahi kuusikia. Mi nshausikia ule uchawi ambao ukipigwa risasi, risasi inakukwepa

hakuna kitu kama hicho!! hii ni burudisha jamii, moto huwa haukosei ukikuandama mwili mzima lazima ufe. kama wachawi wapo wakaibe fedha benki watajirike waachane na umasikini. kama NI KWELI, Leta picha ya tukio tuone.
 
Jaman watu wa jf wabishi uchawi huo upo kuna wezi wengine huwashiki kama unanguo zako yaani huwaoni mpaka uwe uchi chezea uchawi wewe upo sana teh teh teh teh tehte najua mtabisha

kama uchawi huo upo kwanini tusiutumie twende CHINA na MAREKANE tukawaibie mali zao tuzilete bongo na sisi umasikini upungue kidogo!! msidanganyike uchawi wa kihivyo haupo.mchawi wa kiukweli ni ELIMU!!! Elimu imefanya Dunia mahali pazuri ya kuishi.

TV,COMPUTER,SIMU ZA MKONONI,NDEGE vyote ni matunda ya uchawi wa kikweli ELIMU.
 
nasikia Mpanda jamaa aliituma radi ikaunguze benki kwa kuwa alipoteza pesa kwenye akaunt yake, na alipolalamika akajibiwa mbofumbofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…