Je, huu ni ushahidi kiwango cha uaminifu kati ya wananchi kimeongezeka sana hasa kwenye pesa?

Je, huu ni ushahidi kiwango cha uaminifu kati ya wananchi kimeongezeka sana hasa kwenye pesa?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Wakuu kwema?

Niwe mkweli, siku hizi kiwango cha uaminifu kimeongezeka sana hasa kwenye pesa. Sijajua sababu.

Unaweza kukutana na mtu hamjuani ukamuachia pesa nyingi bila maandishi na kazi akafanya tena kwa wakati.

Mifano
Kuna dogo nilimpa 4M simjui anifanyie kazi, bila maandishi, jamaa yangu ananiambia umepigwa, mimi namwambia hakuna nchi imebadilika. Yule dogo kakamilisha kaleta tena kwa wakati. Baadae ananionyesha anapewa kazi na kutumiwa cash mil 20, 5, 8, 3 na kazi zinafanyika bila shida.

Pia soma: Utajiri wako uko kwenye uaminifu, kujituma, na kuweka aibu pembeni

Kwenye bidhaa za kuagiza kwa usiowajua huko ndio raha sana. Jamaa wengi mitandaoni ni waaminifu sana. Nimenunua vitu vingi tena kwa kuletewa nilipo na kitu kinakuja kilekile.

Mfano mtu mmoja alituma bidhaa ambazo kama ningempotezea zingeoza, lakini alituma tena bila hata kumshawishi sana.

Kwa ufupi, kuna mabadiliko sana ya kiwango cha uaminifu katika jamii. Watu wengi wanatumia kama mtaji maana wanajua wakizingua watalala njaa.

Huwa naamini hadi mtu unatapeliwa, huwa kuna viashiria uliviona ukavipotezea. Ila ukiwa mzingativu matapeli ni wachache na ni rahisi kuwagundua ukiwa makini.

Unadhani kwa nini hali imekuwa hivyo?
 
Hata matapeli wanakutengenezea mtindo uwaamini ila ukipigwa mara Moja usijesahau
Sababu kubwa naona kazi zimekuwa ngumu, uwezekano wa kupata mteja umekuwa mgumu, hivyo wenye nia njema wanapopata kazi au tenda au fursa flani wanapambana wafanye vizuri ili wasiharibu. Wapate recommendation.

Ukiona mtu tapelitapeli au sio muaminifu kwenye biashara au kazi kwa kizazi tulichopo hafiki mbali. Pia kuna mifumo mingi sana ya kumdhibiti mtu kama huyo msimu huu
 
Sio wote jichanganye kwangu uone unavyohangaika kutafuta mganga wa kuniroga! Tena na nikijua unatafuta mganga nakutumia tena mganga wa mchongo ili tuendelee kukupiga.🤣
 
sio wote jichanganye kwangu uone unavyohangaika kutafuta mganga wa kuniroga!, tena na nikijua unatafuta mganga nakutumia tena mganga wa mchongo ili tuendelee kukupiga!🤣
Kipindi hiki utafanyia wawili watatu utadakwa tu.
 
Back
Top Bottom