SI KWELI Je, huu ni waraka huu kuhusu uchaguzi umetolewa na TEC?

SI KWELI Je, huu ni waraka huu kuhusu uchaguzi umetolewa na TEC?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
TEC 1.jpg
TEC 2.jpg
TEC 3.jpg
TEC 4.jpg
TEC 5.jpg
 
Tunachokijua
Oktoba 28, 2025 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook imechapishwa taarifa iliyoambatana na kurasa tano ikiwa na utambulisho wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na kudaiw akuwa ni tamko lao kuelekea uchaguzi mkuu unaofanyika leo (Oktoba 29, 2025).

Uhalisia wa Tamko hilo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa tamko hilo halijatolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kama inavyoonekana na badala yake ni tamko la kughushi.

Tamko hilo la Oktoba 28, 2025 limeharirirwa kidogo kutoka kwenye tamko lingine la TEC la kughusi lililotolewa na kusambazwa Oktoba 11, 2025 na kukanushwa na TEC kupitia kwa katibu Mkuu wake Padre, Dkt. Charles Kitima.

Sambamba na hilo, tamko hilo pia limetumia orodha ya Maaskofu ambao wengine kwa sasa hawaudumu kama Maaskofu katika majimbo (katoliki) hayo mathalani Askofu namba 11 kutokea Jimbo la Iringa (Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa) si Askofu wa jimbo hilo tena.

Askofu Ngalalekumtwa aliandika barua ya maombi ya kung'atuka kwa Papa Francisko kutoka katika shughuli za kichungaji kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Iringa nchini Tanzania, January, 28, 2025.

Na baada ya Papa kupokesa maombi hayo akamteua Askofu mpya wa jimbo hilo Padre Romanus Elamu Mihali wa jimbo la Mafinga ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Makamu Askofu wa Jimbo la Mafinga na Paroko wa Ujewa.

Katibu mkuu pia wa baraza hilo Padre Kitima ameeleza kuwa;

"Hiyo ni taarifa FAKE, tulishaitolea ufafanuzi siku za nyuma kuwa ni taarifa FAKE haijatoka kwetu (TEC)."
Back
Top Bottom