Kuna account huko Instagram inafanya biashara ya vyombo vya ndani na jikoni. Huyu bwana anabei inayotamanisha kweli na kwa maelezo yake baada ya kumtwangia simu alidai hana ofisi bidhaa zake zipo nyumbani yeye ukihitaji mzigo anakutumia. Mimi binafsi sikua na shaka na maelezo yake linalonitatiza ni kwanini kafunga comment kwenye Post zake. Je kuna aliyewahi fanya biashara na huyu bwana akapata bidhaa.