Je, huwa unasoma lebo ya bidhaa ukiinunua kabla hujaitumia?

Je, huwa unasoma lebo ya bidhaa ukiinunua kabla hujaitumia?

Superfly

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
985
Reaction score
2,066
Unakuta mtu amenunua kitu dukani, let's say juice, anaifungua, anainywa, bila hata kuangalia namna ya matumizi au expiry date.

Kwa ufupi Watanzania wengi Hatuna utamaduni wa kusoma lebo za bidhaa tunazonunua iwe vyakula au vipodozi...

Lengo la lebo ya bidhaa ni kukupa taarifa zifuatazo.

1. Viambata (Ingredients)

Hapa utafahamu kama kilichotumika kuunda bidhaa husika kitakufaa au hakitakufaa kwa matumizi yako.

2. Expiry date (ukomo wa matumizi)
Hii ni kitu muhimu sana kwani bidhaa nyingi zikiisha muda wa matumizi hugeuka sumu. Kwahyo usipozingatia hili unaweza jikuta unatumia bidhaa ambayo imegeuka kuwa sumu mwilini mwako.

3. Namna ya utunzaji (Storage and handling)

Bidhaa zingine zinakutaka uhifadhi katika mazingira fulani tu, ukikosea bidhaa inaweza kuharibika au kuwa sumu. Mfano yoghurt inahitaji mazingira ya ubaridi, mafuta ya kula na chumvi havitakiwi kuwekwa juani N.K.
Usipofahamu haya utajikuta unatumia bidhaa ambayo ni Sumu!

HITIMISHO
Bidhaa nyingi zinalalamikiwa kuwa na viambata ambavyo ni sumu, mfano case hii ya Juice ya embe ya Azam. Lakin kimsingi "U-Sumu" wa hio bidhaa unategemea na mambo makuu yaliyotajwa hapo juu.. lebo inakupa taarifa zote kisha inakuacha wewe ufanye maamuzi ya kutumia au kutoitumiabidhaa husika. Hivyo ukitumia bidhaa bila kusoma lebo, unajinyima haki yako ya Msingi sana!

Karibuni kwa maoni na Elimu zaidi.
Nawasilisha.
 
Nani anahangaika kusoma maelezo mengi kwa lugha ya kigeni? Halafu halafu lugha ni ya kikemia na kemia wengine hawajui hata a yake. Mwendo ni kubugia tu.
 
Back
Top Bottom