Je, huyu anastahili kumdai mwajiri wake 10% ya NSSF?

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
1,213
Reaction score
1,918
Habarini ndugu!

Kuna mtu kanipiga swali nimeshindwa kumjibu,, yeye alikuwa mfanyakazi sehemu kwa muda wa Miaka 4 na mkataba umeisha juzi Tarehe 31/05/2023.

Amekuwa akiulizia kuhusu kuongeza mkataba kwa muda wa mwezi lakini anaambiwa asubiri.

Jana Tarehe 01/06/2023 akiwa ameenda kuulizia issue ya ajira yake kama ataendelea na kazi akakutana na barua ya KWAHERI kwamba hawana haja naye tena.

Halafu kumbe hakuwahi kuandikishwa NSSF, je huyu anaweza kudai 10% Ile ambayo ilitakiwa mwajiri achangie?
 
Kwanza naomba ujibu maswali yafuatayo kabla sijakushauri.
1. Je mkataba wake umeahinisha wazi kwamba atakua anakatwa % ama muajiri atakua anatoa % kwaajili ya mfuko wa hifadhi..??
2. Salary slp yake inaonyesha kwamba alikua anachangia mfuko wa hifadhi...??
Kama majibu ni hapana na amefanya kazi kwa miaka 5, basi hilo ni kosa ambalo mwajiri wake anatakiwa kuburuzwa mahakamani na mfuko wa hifadhi pamoja na huyo muajiriwa pia.
 
Hii Iliwahi kunitokea Mimi,nikaenda idara ya kazi ndani ya siku 14.mbona nililipwa Hela yangu yote na mwajiri alipigwa faini.
Nenda idara ya kazi chapu mkuu,una Hela za kutosha hapo,miaka mitano?
 
Pole sana nenda CMA......utaoata hakii yako .....ingawa use makini CMA kuna rushwa sana sana .....wana njaa hao ...sikia tu
 
Kwanza naomba ujibu maswali yafuatayo kabla sijakushauri.
1. Je mkataba wake umeahinisha wazi kwamba atakua anakatwa % ama muajiri atakua anatoa % kwaajili ya mfuko wa hifadhi..??
2. Salary slp yake inaonyesha kwamba alikua anachangia mfuko wa hifadhi...??
Kama majibu ni hapana na amefanya kazi kwa miaka 5, basi hilo ni kosa ambalo mwajiri wake anatakiwa kuburuzwa mahakamani na mfuko wa hifadhi pamoja na huyo muajiriwa pia.
Majibu ni HAPANA ndugu, katika mkataba wake hakuna kipengele chochote kinachozungumzia ishu ya MFUKO WA JAMII..
 
Mfuko wa jamiii ni takwa la kisheria hivyo kila mwajiri lazima hakikishe anapeleka 20 percent ya mwajiriwa wake kila mwezi na kama hafanyi hivyo ni kinyume na Sheria hata kama mkataba wake hausemi hivyo na kama alikua amkati alikua anafanya kosa ambalo anastahili adhabu na inatakiwa amlipe Ile asilimia 10 ambayo alipaswa amchangia kwa miaka yote minne
 
Asante.
 
Back
Top Bottom