vitusngitu
New Member
- May 14, 2015
- 4
- 3
Kua bila kukusudiaMsaada wenu tafadhali kuna jamaa mmoja alikuwa na ugomvi na mke wake ndipo yule mwanaume alipoamua kuchukua kipande cha tofali na kumrushia mke wake lakini mama yule alifanikiwa kulikwepa tofali lile na kumfikia mtoto mdogo mwenye miezi mitano.
Baada ya kumpeleka mtoto yule hospitali alipewa referral kwenda hospital kubwa kwa matibabu lakini wakiwa njia mtoto yule alifariki dunia,
Je huyo jamaa atashitakiwa kwa kesi gani kwa kifungu kipi?
atashitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia, pamoja na kwamba awali ilikuwepo transfered malice toka kumdhuru mke hadi kumdhuru mtu mwingine lakini nia ya kudhuru ipo palepale....tatizo linalofanya iwe manslaughter ni kwasababu "death resulting from a fight has to be reduced to manslaughter and not murder". kuna msimamo kama huu wa kisheria umewekwa na mahakama ya rufani.Msaada wenu tafadhali kuna jamaa mmoja alikuwa na ugomvi na mke wake ndipo yule mwanaume alipoamua kuchukua kipande cha tofali na kumrushia mke wake lakini mama yule alifanikiwa kulikwepa tofali lile na kumfikia mtoto mdogo mwenye miezi mitano.
Baada ya kumpeleka mtoto yule hospitali alipewa referral kwenda hospital kubwa kwa matibabu lakini wakiwa njia mtoto yule alifariki dunia,
Je huyo jamaa atashitakiwa kwa kesi gani kwa kifungu kipi?
this is not true brother. kwa mazingira ya kawaida, hapo hakuna pre-meditated intention to cause death which is a prerequisite of an offence of murder. walikuwa wanapigana yeye na mkewe, na akachukua jiwe akampiga mkewe akitarajia kumdhuru mkewe lakini kwa bahati mbaya zaidi jiwe likamkuta mtoto. kosa liko palepale, yaani malice aliyokuwa nayo kwa mama inakuwa transfered kwa mtoto na hali ingekuwa ileile tu kama angedhurika huyo mkewe. ni kitu kilekile tu.Huyo atashtakiwa kwa kosa la mauwaji yaani murder. Wengi wameelezea hapo juu kuhusu men's rea (kusudio la kutenda kosa) na actus reus (kitendo chenyewe). Kwenye sheria haibadilishi kusudio km ulitaka kumpiga A risasi lkn kwa kushindwa kulenga shabaha ukampiga B akafa. Hapo lengo la kuua bado lipo pale pale, ila mlengwa ndo amebadilika.
Ingekuwa manslaughter (kuua bila kukusudia) kwa mfano kama hilo jiwe alitaka kumpiga ndege au kama kifaa alichokirusha kisingeweza kuua kwa mazingira ya kawaida(reasonably) lkn km hicho kitu kingemuua hata huyo mama, haimsaidii kitu km mtoto ndo kafa. Argument nyingine ni kwamba alipaswa kuona kama huyo mtoto angedhurika km huyo mama angekoswa na hilo tofali. (He could have reasonably foresee). Tukumbuke kwamba murder inaweza ikatokea kwa kutenda (commission) au kutokufanya wajibu (omission or negligence). Kuna kesi nyingi za namna hiyo na walifungwa murder. Substitution of malice.
Hayo yote unayoyaelezea hapo itakuwa ni kazi ya mwendesha mashtaka na upande wa utetezi. Hapa mleta mada hakuelezea vitu vyote vinavyoweza kupunguza au kuongeza uzito wa kosa. Kikubwa alichotaka kujua ni kosa ambalo huyo jamaa angeshtakiwa nalo.this is not true brother. kwa mazingira ya kawaida, hapo hakuna pre-meditated intention to cause death which is a prerequisite of an offence of murder. walikuwa wanapigana yeye na mkewe, na akachukua jiwe akampiga mkewe akitarajia kumdhuru mkewe lakini kwa bahati mbaya zaidi jiwe likamkuta mtoto. kosa liko palepale, yaani malice aliyokuwa nayo kwa mama inakuwa transfered kwa mtoto na hali ingekuwa ileile tu kama angedhurika huyo mkewe. ni kitu kilekile tu.
isipokuwa, yapo maamuzi yaliyoweka msimamo kuwa, kifo kinachotokana na watu kugombana kinadondokea kwenye manslaughter. ninazo kesi nyingi kuhusu hilo.
pamoja na kwamba kuna maamuzi yanayosema mensrea inaweza kuangaliwa katika maziringa ya aina ya silaha mtu aliyotumia, eneo alilopiga, amepiga mara ngapi na kwa destruction ya kiasi gani...etc, kama huyo jamaa alirusha jiwe/tofali, actually hiyo sio silaha aliyokuwa nayo kabla ya ugomvi, ilitokea katikati ya ugomvi kutokana na hasira za ugomvi (hapa siendi kwenye provocation), hovyo hatuwezi kusema tofali ni silaha offensive sanaaa katika mazingira ya ugomvi tuliyoyazoea hapa tz, na ikizingatia inayonesha alirusha tofali moja tu na haionyeshi alilenga wapi, kama alilenga kichwani, kifuani,miguuni, mikononi, kiunoni etc hata likampata mtoto.
kama alilenga mguuni, kiunoni na maeneo ambayo sio vulnarable kusababisha kifo kwa urahisi, hapo atakuwa amerahisishiwa kazi. kama alilenga kichwani au kifuani jambo ambalo ni gumu kuthibitisha, anaweza kuhangaika kidogo lakini mwisho wa siku hata kama high court watamfunga, nakuhakikishia court of appeal watakuja na reasoningi kama hizi za kwangu na ataachiwa simply kwasababu kifo hicho kilitokana na ugomvi. watu walikuwa wanagombana.
msimamo ni kwamba, watu wanapokuwa wanagombana, wanakuwa hawana malice aforethought ya kabla, yaani wakati mume anaanza kugombana na mkewe hakuwa na nia kwamba NGOJA NIGOMBANE HALAFU NIMPIGE NA KITU FULANI HADI AFE. nia hiyo ni mara chache inakuwepo kichwani, ndio maana mahakama ya rufaa imeweka msimamo kuwa death resulting from a fight should fall into manslaughter.
however, this could be different kama labda kifo icho kilitokana na kumchoma kisu, (sio tofali), alimchoma sehemu vulnerable kama kifuani, shingoni etc na alimchoma mara nyingi sio mara moja tu na baada ya tukio hakuchukua hatua yeyote kumsaidia victim na mazingira kama hayo. hakuna murder bila malice afore thought, na kuthibitisha malice aforethought ni kazi ya kueleweka kwasababu ikithibitisha murder inataka mtu anyongwe, ndio maana ukiona kuna doubt kidogo tu mshitakiwa anapata faida.