this is not true brother. kwa mazingira ya kawaida, hapo hakuna pre-meditated intention to cause death which is a prerequisite of an offence of murder. walikuwa wanapigana yeye na mkewe, na akachukua jiwe akampiga mkewe akitarajia kumdhuru mkewe lakini kwa bahati mbaya zaidi jiwe likamkuta mtoto. kosa liko palepale, yaani malice aliyokuwa nayo kwa mama inakuwa transfered kwa mtoto na hali ingekuwa ileile tu kama angedhurika huyo mkewe. ni kitu kilekile tu.
isipokuwa, yapo maamuzi yaliyoweka msimamo kuwa, kifo kinachotokana na watu kugombana kinadondokea kwenye manslaughter. ninazo kesi nyingi kuhusu hilo.
pamoja na kwamba kuna maamuzi yanayosema mensrea inaweza kuangaliwa katika maziringa ya aina ya silaha mtu aliyotumia, eneo alilopiga, amepiga mara ngapi na kwa destruction ya kiasi gani...etc, kama huyo jamaa alirusha jiwe/tofali, actually hiyo sio silaha aliyokuwa nayo kabla ya ugomvi, ilitokea katikati ya ugomvi kutokana na hasira za ugomvi (hapa siendi kwenye provocation), hovyo hatuwezi kusema tofali ni silaha offensive sanaaa katika mazingira ya ugomvi tuliyoyazoea hapa tz, na ikizingatia inayonesha alirusha tofali moja tu na haionyeshi alilenga wapi, kama alilenga kichwani, kifuani,miguuni, mikononi, kiunoni etc hata likampata mtoto.
kama alilenga mguuni, kiunoni na maeneo ambayo sio vulnarable kusababisha kifo kwa urahisi, hapo atakuwa amerahisishiwa kazi. kama alilenga kichwani au kifuani jambo ambalo ni gumu kuthibitisha, anaweza kuhangaika kidogo lakini mwisho wa siku hata kama high court watamfunga, nakuhakikishia court of appeal watakuja na reasoningi kama hizi za kwangu na ataachiwa simply kwasababu kifo hicho kilitokana na ugomvi. watu walikuwa wanagombana.
msimamo ni kwamba, watu wanapokuwa wanagombana, wanakuwa hawana malice aforethought ya kabla, yaani wakati mume anaanza kugombana na mkewe hakuwa na nia kwamba NGOJA NIGOMBANE HALAFU NIMPIGE NA KITU FULANI HADI AFE. nia hiyo ni mara chache inakuwepo kichwani, ndio maana mahakama ya rufaa imeweka msimamo kuwa death resulting from a fight should fall into manslaughter.
however, this could be different kama labda kifo icho kilitokana na kumchoma kisu, (sio tofali), alimchoma sehemu vulnerable kama kifuani, shingoni etc na alimchoma mara nyingi sio mara moja tu na baada ya tukio hakuchukua hatua yeyote kumsaidia victim na mazingira kama hayo. hakuna murder bila malice afore thought, na kuthibitisha malice aforethought ni kazi ya kueleweka kwasababu ikithibitisha murder inataka mtu anyongwe, ndio maana ukiona kuna doubt kidogo tu mshitakiwa anapata faida.