Hivi mkuu dini ni nini? Na una maoni gani kuhusu hoja ya kutenganisha dini na Mungu?
Umeuliza Maswali mawili Na nitayajibu!
Japo maswali yako yanaweza Kuonekana machache iola majibu yake yanaweza Kuchukua Kitabu Kizima Chenye Kurasa 800 au 1600 na Kituk 😀😀
Tafsiri Sahihi ya Neno Dini!
Neno Dini limetoka na Neno la Kiarabu الدين (ad-dīn),
Lenye maana Ya Mfumo mzima Wa Maisha...
Yaani Daily Routine kwa Kingereza..
Kwa tafsiri ya Kiswahili ningesema Jinsi Unavyoamka Asubuhi Vitu unavyofanya Mpaka Unavyolala Tena Usiku..
Yaani unaishije unajumuila Vipi na Watu unafanya nini..
Na ndo maana Katika Uislamu Wanaamini Kuwa Kila Kitu ni Ibada kuanzia Unavyoamka mpaka Unavyolala..
Sasa Kwa Muktadha Mwingine Dini Hutafsiriwa Kama Njia (Kwa lugha hiyo hiyo ya Kiarabu) yaani Njia nikimaanisha Hatua Zote utakazochukua Ili Kufikia Lengo fulani Huitwa Din..
Kwa mfano Ili niweze Kufaulu Chuo nahitaji kufanya Njia Fulani Ili niweze kupata Bachelor Degree au Master Degree au Doctorate Degree..
Sijui Kama Nimeeleweka hapo..?
Swali la Pili Nina Maoni Gani ya Kutenganisha Dini na Mungu...
Kwa Mfano!
Kwa Wayahudi, Wakristo,na waislamu (Ibrahimic Religion)
Huamini Kuwa Musa Ndiyo njia Sahihi ya Kufika Kwa Mungu Na wao Huzichambua Sheria za Musa Na torati kwakuwa wanaamini Ndizo walizoachiwa na Mungu kupitia Musa na Yoyote atakayezipinga kwao humuona Mkosaji Haswaa na Kafiri..
Wakristo wao Huamini Kuwa Yesu Kristo Ndiyo Njia sahihi ya Kufika Kwa Mungu na wao Mtu yoyote asiyefata Mafundisho ya yesu humuona kama Kapotea..
Kama
Yohana 16:4 inavyosema..
Lakini Yesu Pia aliwahi Kufafanua Mwenyewe Kuhusu Nini maana Ya Uzima Wa Milele ambayo na yenyewe inafanana sana Na Ila
Kalima Shahaadat au
Ushahidi wa Imani wa Waislamu..
Ambao ukisoma Kwenye Biblia Yesu badala ya Kuuita Ushahidi wa Imani au Shahada ametumia Neno Uzima Wa Milele..
Tito 1:2
"katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele;"
Au kama Yeye mwenyewe AlivyoUtafasiri.. Yohana 17:3
Ukiangalia Kauli Hiyo Utaona Ina pande Mbili..
Pande ya Kwanza ..
- Kumjua Mungu Mmoja na wa Pekee na wa kweli
Kauli hii Uliifatilia Utagundua inafanana na Kauli Iliyowahi kusemwa na Musa Pia kauli Hii Hutumika kama Tamko la kiimani la Kiyahudi, wao Wanaita
Shema Yisrael (שְׁמַע יִשְׂרָאֵל)..
Au kwa Urefu "Shema Yisrael, Adonai Eloheinu, Adonai Echad"
Ambayo Tafsiri yake ni "Sikia, Ee Israeli: Bwana Mungu wetu, Bwana ni Mmoja."
lakini Kauli Hiyo Pia Unaweza Kuipata Kwenye Dini ya Kiislamu kama nilivyosema Awali kwenye Kalima shahaadat ya Kwanza ambayo ni tamko la Tawhud kwa wale waislam ambalo ni
La ilaha illallah (لَا إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّٰهُ).. yaani
"Hakuna mungu apaswaye Kuabudiwa ila Allah."
Kauli hii Inamuonyesha Yesu kama Njia ya kufika kwa HuYo Mungu mmoja Kwa sababu yeye ndiyo aliyetumwa ns Huyo Mungu iko sahihi kabisa na Inamfanano kabisa na Kauli ya Kalma shaahadat ya Pili..
Muhammadur Rasulullah (مُحَمَّدٌ رَسُولُ ٱللَّٰهِ) ambayo inamaanisha:
"
Muhammad ni Mtume wa Allah." Au "
Muhamad Aliyetumwa na Allah"
Sasa Kwa Kauli hizo mbili Maana yake ni Ipi sasa Ni kwamba Waislam wanaamini Ili Kuweza Kufika kwa Mungu Lazima Upitie njia ya Mtume Muhamad kwani yeye ndiye aliyetumwa na Mungu na Yesu alitumwa Pia Ila kwa zama tofauti..
Na Wakristo wanaamini Kuwa Yesu ni Mkombozi aliyetumwa na Mungu Kuja Kukomboa Taifa kutokana na Dhambi zao..
Vipi Kuhusu Wahindu na Bhagavad Gita
Ukisoma Kweny kitabu Kitakatifu cha wahindu Bhagavad gita:.. (Chapter 9 verses 18)
krishna akimwambia Arjun krishna alitamka kuwa yeye Ndiyo Njia ya Kweli na Uzima maneno yaliyosemwa Na yesu Miaka kadhaa Baadae..
"I am the way, the life ,the sustainer,the Lord ,the witness,the abode, the refuge and the most intimate friend. I am the creation and the dissolution, the basis of everything, the resting place and the eternal seed.."
(Mimi ni ni Njia,uzima, Muongozaji,Bwana,Shahidi, Mnyenyekevu, Mwokozi,na Rafiki wa karibu,Mimi ni Uumbaji,na Uharibifu,mimi ni Mwanzo wa kila kitu , Sehemu ya Pumziko na Mbegu (Chachu) ya milele.)
Unaweza Ukaona
Tz mbongo hali Inavyochanganya Kwahyo Who to trust Ikiwa Kila Mmoja anaushahidi wa Ayafanyayo na kumuona Mwenzake Hafai?
sasa ili kutengenisha Dini na Mungu unatakiwa Kutumia Hekima Kubwa sana ikiwemo Kuamini Kuwa Mungu Ni upendo kama Alivyojisema yeye Kwenye Dini zote..
Na Uchukue Intersection ya Mafundisho Ya Dini zote yaani Mambo ambayo yanafanana Kwenye Dini zote Ndo yawe Muongozo wako Na yale yanayopingana Yaweke Kando Songa Mbele..
Na Hiyo Ndiyo Dini safi..
Na Unaweza Kutenganisha Dini Na Mungu kwa Muktadha huo..
Najua unaweza ukasema Kuwa Ungejuaje Mungu bila Kujifunza Kutumia Dini sasa Itakuwaje tena Useme Dini Haziwezi..
leo hii wewe ni Engeer, Daktari, Rubani ,Mtu msomi sana..
lakini Usisahau Ulifundishwa na Mwalimu ambaye Huenda alikuwa Ni wa UPE au Alikuws ni Form four na Alisoma Course ya Ualimu baada ya Kufeli..
Je Baada ya Kukufundisha wewe Na Wewe Kuwa Daktari au Kuwa Rubani Does It make Him Proffesor? Au Does it Make Him Mwenye Elimu Kukuzidi?
hapana Itamfanya Kuwa Hero kwa kuwa Umetoka kwenye Mikono yake japo Umekuwa Mkubwa kielimu kumzidi yeye..
na ndiyo Dini ilivyo.....
dini Hutufikisha Sehemu ambayo Tunatanuka Mawazo na Kujua Vingi Ila baada ya Kujua Vitu hivyo dini Haiwezi kuwa Kubwa Kuliko mawazo yetu sisi..
so Dini Na Kumjua Mungu na Dini na Mungu ni Vitu viwili Tofauti
CC;
Aaliyyah