Je, inawezekana kumpenda mtu deeply bila kumuona?

that manzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
385
Reaction score
1,246
Habari ya jioni wakuu katika Jf, poleni na hongereni kwa hekaheka za siku ya leo..

nimekaa hapa nikarafakari nikajiuliza nikakosa majibu imebidi nililete kwenu naombeni kuuliza wajuzi wa mambo mnijuze…
Je ni kweli inawezekana ukampenda mtu ambae hujawahi kumuona? like labda unaskia tu sauti yake? nazungumzia ule upendo kimapenzi yaaani mtu unaweza ukafall deeply kabisa?

Inawezekanaje? hebu ambao mlishawahi kufall au kupenda mtu kabla hamjaonana mje mtupe story ilikuaje na nini kilitokea

Je huo upendo huwa unaongezeka au unapungua baada ya kuonana?

 
Naonaga ni uongo tu huo, hamna ile real connection, mtakua mnapendana ila sio upendo wa kweli hasa kwa Me, ila Ke wanapenda kweli sometimes ila mwanaume akwambie kakupenda na hamjawahi kuonana (kwa sauti tu), anakupiga kamba huyo hatupogo hivyo sisi.
 
Nilipokuwa kijana mara nyingi nilishindwa kuunganisha mapenzi kwa sauti ya mtu na sura yake.

Iko hivii, nilikuwa switch board operator enzi hizo, saazingine ilitokea kuvutiwa sana na sauti za baadhi ya wasichana kwenye simu na mara zote nilipomfuatilia mhusika sikuvutiwa naye hata kidogo!

Baadaye nilikuja ku conclude kwamba wasichana wenye sauti nzuri sana, hawana mvuto kwangu, nikaishia hivyo.

Lakini suala la teknolojia mpya ya mitandao kama tunavyoandikiana sasa hivi nadhani kuna tofauti kubwa.

Kwa namna ninavyovutiwa sana na thread ama comments za baadhi ya wanawake humu Jf, nadhani nikionana nao ana kwa ana siwezi kuanza kutathmini tena sura, naoa.

Kwa sababu hufurahishwa na kuvutiwa sana na mwanamke mwenye 'madini' kichwani kuliko misura.
 
duuh
 
Naonaga ni uongo tu huo, hamna ile real connection, mtakua mnapendana ila sio upendo wa kweli hasa kwa Me, ila Ke wanapenda kweli sometimes ila mwanaume akwambie kakupenda na hamjawahi kuonana (kwa sauti tu), anakupiga kamba huyo hatupogo hivyo sisi.
kwa kweli hata me sielewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…