monde arabe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 8,781
- 13,444
Habar za Leo ndugu wanajukwaa,
Siku chache zilizopita nilienda kwenye tawi la bank Moja maarufu hapa nchini kwaajili ya ku-process mkopo kutoka kwenye bank hiyo.Afisa mikopo alinipigia mahesabu na ikaonekana kuwa naweza kupata kiasi cha zaidi ya milioni tisa za Kitanzania.Leo nikampigia cm Afisa yuleyule kuhitaji kiasi kilekile na kwa muda uleule (muda wa kurejesha mkopo)
Nilishangaa sana!!!! jamaa ananiambia kuwa naweza kupata kiasi cha shilingi milioni Moja na laki tatu tu (1,300,000/=) nikikopa kiasi kilekile,na nikirejesha Kwa muda uleule.Nikahisi kuwa huenda huyu mtu mwanzo nilipoenda wiki mbili zilizopita anaweza kuwa alikopa kwa kutumia taarifa zangu course anazifahamu hatakama sikumpatia mimi bado aweza kuwasiliana na Afisa utumishi na kuzipata.
Wenye elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya kibenki,mikopo,fedha na uchumi naombeni mnipe elimu ndugu yenu...kutoka kupata milioni tisa Hadi milioni moja na laki tatu siyo poa.Pia,nitawezaje kujua kama alikopa kwa kutumia taarifa zangu?
Na ikitokea nimejua kuwa huyu Afisa mikopo alikopa kwa kutumia taarifa zangu je,nifuatilie kwa kutumia utaratibu gani?
Naomba kuwasilisha!