Je, inawezekana mtu akalala na mwenye UKIMWI tena peku na asipate UKIMWI?

Nina rafiki yangu ameoa miaka mitatu iliyopita mwaka huu ndiyo anakuja kujua kuwa mke wake anaukimwi, wana mtoto mmoja. Alikuja kukuta vidonge ARV ndani kwenye bag la mke wake, kumuuliza ndiyo anamwambia kuwa yeye (mke) ni mgonjwa.
Jamaa alichanganyikiwa asijue cha kufanya, siku iliyofuata alipokuja kazini akaanza kuwambia baadhi ya wazee kazini hali aliyoikuta nyumbani, walimkalisha chini, wakiwa wanamshauri kuwa usichukue maamuzi yeyote magumu, kubaliana na hali, maisha yataenda.
Wakamwambia sasa jitayarishe kisaikolojia, twende ukapime ili aanza kutumia dawa, jamaa akakubali.
Kwenda kupima hakukutwa na maambukizi yeyote. Kutokana na hiyo hali akawashirikisha familia zote mbili, wakakubaliana yeye, mke wake na mtoto wakapime tena kujua ukweli wa hayo.
Majibu yakatoka kuwa ni mama tu ndiye mwenye maambukizi, baba na mwanaye wako safe .
Wamepima Mara kadhaa majibu ni hayo hayo.
Nawauliza madaktari na wenye elimu kuhusu hili gonjwa la ukimwi hii hali inawezekanaje?
 

ngoja wakuu waje na majibu japo kua yamesha jibiwa sana tu umndani
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mkuu, naomba tupe elimu hii, ni kweli Kuna watu wengi wakiacha kutumia dawa wanaondoka, nini kifanyike ili mtu akiacha dawa aendelee kudunda kitaa
 
Deception....
Sasa hii ni nini?
Mbona watu wanakufa kwa huu ukimwi?
Na ukiupata unaponaje?
 
Huu uzi nimeufuatilia mwanzo mwisho kwakweli nimepata cha kujifunza,.. Ila tatizo ni kumweleza mtu akakuelewa ni jinsi ya uwakilishaji wako wa maelezo na ushahidi kama ndugu yetu Deception... Hongera sana Mungu akubariki.
 
Wewe ni zaidi ya MPUUZI..!
Unamshambulia mtu badala ya kushambulia hoja zake(ambazo kwako ni upotoshaji) kwa kutoa hoja zako(unazoamini ndio kweli)..!
JINGA kabisa wewe..!
 
Deception anayoyazungumza ni kweli kabisa,MIMI hapa Nina miaka 23 na nimezaliwa nikiwa na HIV sijawahi kutumia ARVs na Niko vizuri na cd4 zangu ziko juu na kwa niliyoyasoma hapa haki ya mungu situmii dawa ng'oo
VIP ulipiwa ukiwa umezaliwa je ivi karibuni umepima tena uenda vipimo vilikosea
 
Mi nilipima 2015 nipo + ila nimezaliwa nao family ilikua haijanambia,2016 nikachek cd4 ziko juu Dr akanambia nichukue dawa nikagoma (nilikua bado sina elimu yoyote kuhusu hayo madawa ila nilikataa maana muoga wa dawa) nikamwambia Dr zikishuka nitakuja sasa nikawaza kama nimeweza kuishi zaidi ya miaka 20 bila mapipi yao kwanini nitumie sasa,nikichanganya na niliyosoma humu yaani labda wanizimishe halafu ndo wanipe
 
Niongezee kidogo. Niliishi na mke wangu miaka kumi. Alianza kuumwa mwaka wa nane wa ndoa yetu. Nilipuuza. Mwaka wa tisa nikaanza kupata hofu baada ya kusikia aliyekuwa mpenzi wake kabla yangu ana virus. Hatukupima hadi alipozidiwa mwaka wa kumi. Nilimpeleka hospital ambapo walimshauri apimwe na majibu yakawa +. Akafa siku iliyofuata kwa hofu.
Niliishi kama mwaka hivi nikaamua nikapimwe. Sikuamini niliambiwa sina maambukizi. Nilirudia zaidi ya mara tano kwa kubadilisha vituo lakini jibu likawa ni -
Hadi leo najiuliza imewezekanaje, sipati jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…