Mkuu
Deception ni kweli kabisa siyo wote watakuelewa na siyo wote watafuata kile unachosema. Sababu ni kwamba watu wengi hatuna kasumba ya kusoma zaidi ya kile tulichofundishwa, pia hatuna kasumba ya kuuliza nje ya kile tunachofundishwa. Mimi sina hata chembe ya udaktari, lakini haya matibabu ya asili nimeanza kuyafuatilia baada ya kuanza kujiuliza maswali mengi bila kupata majibu ya maana, nikawa na interest ya kusoma zaidi habari zake ndo nikagundua ni kinga nzuri tu.
Hizi dawa au kinga asili zinatumika pia hata kwenye mifugo. Kule jukwa la biashara kuna uzi umegusia tiba za asili. Sasa mimi kwa vile tayari nazitumia, sikupata tabu kuamini kuwa zinafaa kwa mifugo pia. Kifupi mi nafuga kuku, wachache tu kama mia hivi wa kienyeji kwa matumizi ya familia. Hawa kuku natumia sana kinga asili na wako poa, magonjwa ya mlipuko yanaibuka kuku wajirani wanakufa wangu wapo tu, nikiwaambia nachotumia hawaamini wanabaki kunishangaa tu. Ila napo inapotokea ugonjwa fulani naanza na hizi za madukani zinazofanya kazi fasta then naendelea na asilia zangu kama kawaida. Tena hata hivyo nimekunja kugundua magonjwa yanaibuka pale ninapozembea kuwapa kinga za asili au ninapokuwa nimesafiri kwa muda mrefu waliopo wakazembea kuwapa. Lakini ukiifanya kama sehemu ya diet mbona magonjwa utayasikia kwa jirani tu.