anti-negative energy
Senior Member
- Apr 13, 2019
- 114
- 71
WANAJAMVI, hebu leo tujumuike kujadili hili swala la barabarani ambalo imekua kero kwa muda mrefu sana. Kitu kimoja ambacho mimi huwa kinanitia hasira ni jinsi traffic wanavocontrol juntion kwa upendeleo, yani kama wale tunaopita njia ya morrocco kwa kuelekea kawe ni matatizo mkuu, unaweza kukaa kwenye junction hata masaa mawili, unaambiwa barabara kuu(BAGAMOYO ROAD) ndo inayopewa kipaumbele au kiongozi anapita.
Sasa mm huwa najiuliza kitu kimoja, inamaana mamlaka ya usafiri imeshindwa kua na ubunifu, kwa maana ya kwamba badala ya kusimama trafic( ambaye sometimes anaweza akawa anafanya makusudi wenda kwa sababu ya stress za mke wake nyumbani) kwanini wasijaribu kuset zile traffic light ili kama bagamoyo road imepewa kipaumbele basi waweke mda unaojulikana. kwa mfano bagamoyo road inaweza ikawekewa hata dakika zisizozidi 5 na njia nyingine zitembee. hata kama wakiongezea mda barabara kuu hatukatai ila uwe mda unaojulikana.
Kwa sababu matrafic wanaoongoza haya magari hawana wasimamizi na vile watanzania tusivojua kupigania haki basi unaweza kuta foleni inasubilishwa mda wowote anaotaka traffic. Traffic akiamua kukuweka kuanzia asubuhi hadi jioni, watu wanaishia kunongona tu lakini hakuna reaction yoyote. na upotezaji wa mda barabarani ni jambo ambalo watanzania wengi tunaanza kulichukulia poa. yani ukiishi dar its very stressful kwenye swala zima la kua ontime kwenye shughuli zako.