second9
JF-Expert Member
- Jun 22, 2016
- 216
- 451
Wakuu nimejaribu kutafakari kidogo kwa haraka, pamoja na uwepo wa Mheshimiwa Doto Biteko kama msaidizi wa waziri mkuu wa sasa Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Naona bado kuna namna Mheshimiwa Bashungwa anaandaliwa kwa nafasi ya uwaziri mkuu. Nikiangalia ni kama anapitishwa hizi wizara mbalimbali ili aweze kuzitambua namna zinavyofanya kazi maana kwa muda huu mfupi anaopita kwenye wizara ni ngumu sana kufanya mabadiliko chanya kwenye kila wizara.
Hizi ni wizara alizopita kwa muda usiozidi miaka 10:-
Sina kabisa interest na CCM ila sina shaka sana na utendaji kazi wa huyu bwana mkubwa aliyezaliwa 1979 huko wilayani Karagwe, mkoani Kagera.

- 2018-2019 - Naibu Waziri Wizara ya Kilimo.
- 2019-2020 - Waziri wa Viwanda na Biashara.
- 2020-2021 - Waziri wa Habari, Sanaa, na Michezo.
- 2022-2023 - Waziri wa TAMISEMI.
- 2023-2024 - Waziri wa Ulinzi.
- 2024-2025 - Waziri wa Mambo ya Ndani