Biashara ya udalali inahitaji uvumilivu mkubwa, hasa kwa madalali wapya wanaofanya kazi miongoni mwa madalali wenye uzoefu mkubwa wa kazi. Ili kuwa katika njia sahihi, dalali mpya lazima atambue na kuzitumia vyema fursa mpya zinazojitokea.
Dalali mpya azungumze na madalali wenye idadi kubwa ya nyumba au viwanja vya kuuza au kukodisha. Pia, kumbuka fursa kama haijitokezi basi inabidi zitafutwe kwa namna yeyote ile. Ukipata wateja, hakikisha unakuwa na wakati wa makubaliano ili ujifunze na kuonesha nia ya kufanya kazi kama dalali. Madalali wenye uzoefu wakikuamini kuwa unaweza kuwaletea wateja, basi itakuwa rahisi kukutafuta wakiwa na nyumba au kiwanja kingine. Na huo ndio utakuwa mwanzo wako mzuri.@Kitomai