JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Upangishaji wa nyumba au chumba unaendeshwa na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 , ambapo sheria hiyo imetaja wahusika wawili tu katika upangishaji.
Wahusika hao ni mpangaji na mpangishaji, sheria hii haijataja nafasi ya dalali, hivyo dalali anakuwepo kwa makubaliano kati ya mpangishaji au mpangishwaji.
Kwakua dalali yupo kimakubaliano ya mmoja wapo kati ya wahusika wawili, makubaliano hayo yataendeshwa na sheria ya mikataba.
Hivyo kwenye sheria hiyo dalali anatambulika kama wakala.
Ambapo wakala ni mtu aliyeajiriwa kufanya kitu chochote kwa niaba ya
mwingine, au kumuwakilisha mtu mwingine katika shughuli mbalimbali.
Mtu ambaye anafanyiwa shughuli hizo au anayewakilishwa anaitwa "mhusika mkuu".
Upvote
1