Je ipi ni sahihi?

Sasa Niah
Pale unapokuta pameandikwa ke kama kifupi inakuwa inamaanisha nini kwa maana mwanaume na wakiume vyote vyaishia na me mmmhh ...Ikoje hapo Niah wangu
hapo niah hawezi jibu atakwepa
 
Sasa Niah
Pale unapokuta pameandikwa ke kama kifupi inakuwa inamaanisha nini kwa maana mwanaume na wakiume vyote vyaishia na me mmmhh ...Ikoje hapo Niah wangu
Unajua Zuleykha, huwezi andika kila kitu kwa kilefu. Tunaandika Bw. Bi. Dr. Mh. hii yote ni kufupisha. Njia nyingine kama vyoo hawandiki hata Ke wala Me bali kuna picha ya kike na ya kiume na choo ambayo watoto wanabadilishwa unaona picha ya kitoto kwenye kitanda cha kubadilishia. Ukienda kwa kizungu wenyewe wanatumia F na M badala ya kurefusha maneno hayo. Ni mitindo tu ambayo baadaye imekuwa kama kanuni ili kuokoa muda na space.
 
Jinsia ni mbili tu jinsia ya kike au jinsia ya kiume

Hakuna jinsia ya mwanamme au jinsia ya mwanaume
 
Jinsia ni mbili tu jinsia ya kike au jinsia ya kiume

Hakuna jinsia ya mwanamme au jinsia ya mwanaume
Sawa mtoto wa kiume utamuita kama alivyo , je wewe apo ni wakiume au mwanaume?
 
Kwa hiyo Niah utakubali kuitwa wakike au utakubali kuitwa mwanamke?
 
Na mwanao utamwita mtoto wa kike au mwanamke?
 
Kwa hiyo Niah utakubali kuitwa wakike au utakubali kuitwa mwanamke?
Mimi bibi lakini nilipokuwa kigori au mdogo ningetaka siyo kupenda niitwe msichana au mtoto wa kike. Baada ya kuolewa ukiniita wa kike ni tusi unaniangalia halafu unasema mwanamke wewe hujambo ambavyo navyo si safi tuna lugha ya haiba ya kuita. Bibie hujambo, mama, mama fulani. Ukisikia mtu anaita wewe mwanamke ujue ni shari. It is too formal. Isimu/stylistics and syntax ni masomo magumu sana ndiyo maana watu wengi huwa wanayakwepa wanapofika mbele.
 
Na mwanao utamwita mtoto wa kike au mwanamke?
We mwana we! Mwanangu tena nimuite mwanamke. Nikiulizwa mwanangu jinsia gani nasema YA kike meaning sisemi mwanamke. Huulizwi una wanawake na wanaume wangapi bali una watoto wangapi wakike na wakiume? Note the difference. Bwana naenda kupika iliza nikiwahi nitasoma. Saa za msosi hapa kwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…