Je ipi ni sahihi?

Je ipi ni sahihi?

Zuleykha

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Posts
1,247
Reaction score
1,815
Habarini wanajamvi.
Hakika hili lanitatiza,na ninaamini hapa ndipo penyewe.Ni hivi;
Mtoto anapozaliwa na kukutwa anajinsia ya kike.
Tutasema kazaliwa mtoto wa kike au kazaliwa mwanamke?
Nawasilisha
 
Kazaliwa mtoto wa kike ndo sahihi

mwanamke ni yule alievunja ungo....na kuwajua wanaume

kabla ya hapo unakuwa mtoto wa kike halafu unakuwa msichana

ukishabikiriwa ndo unakuwa mwanamke

ndo maana wanasema 'amemuondoa usichana wake'
 
Nimekuelewa .Lakini neno mwanamke ni muunganiko wa maneno mawili mwana na mke je? waweza fafanua hapo?
 
Mtoto anapozaliwa na kuwa na jinsia ya kike, Ukisema "wakike" mwingine akasema "mwanamke" wote mko sahihi.

Tunaposema mwanamke tunaangali jinsia bila kujali umri wake.

lakini tunaposema "wakike" tunadogosha.

kwasababu neno mwanamke lina umbo litokanalo na maneno matatu " mwana + mwenye + uke = mwanamke.

mwana +mwenye + uume = mwanamme
 
Siungi hoja mkuu. Kama the Boss alivyoainisha ndivyo ilivyo. Je ukiwa unataka kumwita mtoto wa kike usiyomfahamu jina waweza mwita "we mwanamke njoo hapa". Huwezi, utasema wewe msichana au dada njoo hapa. Kiswahili si tajiri wa maneno kama lugha nyingine ndo maana sisi tuna mtoto wa kike lakini kama waingereza watasema a Girl. Wana baby girl, a young girl and a girl. Sisi msichana au kama mdogo hatusemi mtoto wa kisichana bali tunasema mtoto wa kike.
 
Unajua mazoe yanaweza kukufanya uhisi makosa uliyozoea kuzungumza ndio usahihi wenyewe !!

Naendelea kusisitiza kusema wa kike ni kudogosha !

Nenda kwenye kamusi uone maana ya Leksimu Mwanamke halafu njoo !
 
niah mtoto wakike anapozaliwa kwenye cheti cha kuzaliwa ile KE inawakilisha mini? Mwanamke au Wakike ?
 
Ke si kifupi na wewe? Ulitaka kwenye form waandike neno lote mtoto wa kike? Ndiyo maana wenzetu sababu ya kuwa na msamiati mkubwa wanatumia F na M wakimaanisha Female and Male. Hii ni kwa rika lote. Sisi hatuna maneno mengi ya kutwist lugha ndiyo maana wanaweka Ke na Me. Hivyo mtoto wa kiume aitwe mwanaume vile? Unaisikiaje masikoni mwako. We mwanaume njoo hapa! Si unaita wewe kijana au wewe mvulana njoo nikutume?
 
Naona unaanza kuelewa sasa !!

sasa mini kirefu cha hiyo KE?
 
Mazoea yana tabu niah

mfano wewe unaitwa niah moghasa sasa hilo jina lako badilisha ujiite moghasa niah !!!!

utaona kama sio sahihi
Mazoea na uhalisia ni vitu mbali mbali. Yaani tusiache lugha iparaganyike eti sababu ya mazoea. Kama umegundua watu wengi utawasikia wanasema hili neno "wamama" au "wababa". Na huu mchezo ulianzishwa na hawa walokole kuchanganya lugha zao za asili na kiswahili. Ikaja hii ya "mimi huwaga simwogopi huyo", kisa wasukuma wengi nchini hivyo kila mtu akaanza. Tujitahidi kuongea kiswahili sanifu ili kiweze kusonga mbele. Wale wanaosoma bado unadhani wakiandika mwanamke badala ya mtoto wa kike watapata maksi? Nikimsahihisha huyo namkata kabisaaaaaa.
]
 
Mtoto anapozaliwa na kuwa na jinsia ya kike, Ukisema "wakike" mwingine akasema "mwanamke" wote mko sahihi.

Tunaposema mwanamke tunaangali jinsia bila kujali umri wake.

lakini tunaposema "wakike" tunadogosha.

kwasababu neno mwanamke lina umbo litokanalo na maneno matatu " mwana + mwenye + uke = mwanamke.

mwana +mwenye + uume = mwanamme
Inamaana neno mwanamke limeundwa na maneno matatu?
 
Ke si kifupi na wewe? Ulitaka kwenye form waandike neno lote mtoto wa kike? Ndiyo maana wenzetu sababu ya kuwa na msamiati mkubwa wanatumia F na M wakimaanisha Female and Male. Hii ni kwa rika lote. Sisi hatuna maneno mengi ya kutwist lugha ndiyo maana wanaweka Ke na Me. Hivyo mtoto wa kiume aitwe mwanaume vile? Unaisikiaje masikoni mwako. We mwanaume njoo hapa! Si unaita wewe kijana au wewe mvulana njoo nikutume?
Sasa Niah
Pale unapokuta pameandikwa ke kama kifupi inakuwa inamaanisha nini kwa maana mwanaume na wakiume vyote vyaishia na me mmmhh ...Ikoje hapo Niah wangu
 
Back
Top Bottom