Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 3,230
- 6,742
Niliwahi kuhudhuria ibada ambayo mchungaji Peter John wa Kanisa la Waadventista Wasabato alihubiri na kufundisha kuhusu Taifa la Mungu ndio nikaelewa vyema kuhusu suala la Israel
(nitajitahidi kutafuta lile hubiri kwenye youtube natumai itatusaidia wengi kwani tangu baada ya hapo uelewa wangu umekuwa tofauti sana kuhusu Israel)
Kwa kifupi alihubiri hivi (mtaniwia radhi ikiwa ntaiwasilisha isivyo maana nilisikiliza tu sikunukuu popote)
Mungu aliiumba hii dunia akiwa na lengo maalum na hutumia watu kwa ajili ya kutimiza kusudi lake la kuiumba dunia hii, (hapa alinukuu Mwanzo na vifungu vile vya binadamu kuijaza dunia na kutawala vilivyomo)
Hivyo huchagua mtu maalum kwa ajili ya kutimiza kusudi lake na kuwafikishia ujumbe wake kwa watu wote ili lengo lake litimie (manabii, mitume etc.)
Yoyote anaechaguliwa na Mungu sio kwamba yeye ni bora sana kuliko wengine bali hutumika kama chombo ili kufikisha kusudi kwa watu na akatoa mfano wa bomba akasema sio bomba ndio linalokata kiu bali ni maji yanayopita ndani yake
Unaweza kutandaza bomba kuanzia Dar mpaka Songea lakini isiwe na faida yoyote ikiwa hayatapita maji ndani yake
Hivyo wana Israel ni kama Bomba ambalo lilichaguliwa na Mungu ili kupitisha hayo maji ya uzima ili habari imfikie kila mtu hatimae wote wapate kuokolewa na ndio ahadi ya Mungu kwa Abrahamu Baba wa Taifa la Israel kuwa atamfanya Taifa Kubwa na kila ataembariki atambariki na kila atakayemlaani atalaaniwa na kupitia yeye mataifa yote watabarikiwa
Kitu bora sio watu wa Waisrael ila ni ule ujumbe ambao Mungu aliupitisha kwa wana Israel ili uwafikie wote Ulimwenguni
Wao wanachokosea (sio wote) ni kujiamini kuwa wao ni bora sana kuliko wote na kusahau ujumbe ambao walipewa ndio jambo la msingi zaidi, na kuwa lengo la Mungu ni yeye atukuzwe na sio binadamu hivyo kwa chochote chema sifa, shukrani na utukufu ni vyake daima
Je ukichaguliwa halafu ukawa unakosea utabaki hivyo hivyo? Hapana ni lazima uendelee kutii maagizo ya Mungu ili kuwa mchaguliwa, na ndio maana hata Yuda alichaguliwa kuifanya kazi ya Mungu ila baada ya kuasi kibali kiliondolewa nafsini mwake
Hivyo kuwa mkristo au mtu mwengine yoyote yule hakukusaidii kitu ikiwa hufati maagizo ya Mungu ya kumtukuza na kumkiri kuwa yeye ndio muweza wa yote na ndio kaiumba dunia hii, kuyafata mapenzi yake yote, kutotegemea miungu mingine, kupendana etc.
Hiko ndio nilichopata ila natumai ukitafuta mafundisho mbalimbali kwenye mtandao kuhusu suala la Israel utakutana na wachungaji au wahubiri ambao wamefafanua zaidi na utaelewa msingi wa imani ya wakristo wengi juu ya Israel kuwa Taifa la Mungu