Mtoto; kibaiolojia atabaki kuwa na Baba mmoja, Mama mmoja.
Kimazingira, anaweza pata Wazazi walezi kwa kadiri ya mazingira atakayokutana nayo/yaliyomzunguka. Huyo baba, amlee au la, ni jukumu la mtoto kuja kuamua amuweke nafasi ipi Mzazi wake huyo atakapokuwA amefikia umri wa kung'amua mambo.
Si jukumu la mama kumtenganisha mtoto na baba, wala usijaribu kummezesha SUMU, inaweza kukugeukia siku za usoni au kumuharibu mtoto mazima.
Itategemea na malezi utakayompa sasa, malezu hayo ndio jibu la swali lako siku za usoni.
Mama, mlee mwana, ni mwana toka tumboni mwako.