Sasa mkuu tusipo tumia "huenda" wewe unawakikika bila kuleta ushahidi wa maandiko kwamba tafsiri yako kuhusu hilo la Paulo kua muongo? probability sentence ni lazima itumike paka pale utakopo bainisha kwamba Paulo alitumia lugha ya mafumbo kumanisha hilo aliko sema, ila otherwise tutachukua maneno yake kama yalivo kwasbabu na maneno ya bibulia yote huchukiliwa hivo hivo..... wewe unaleta scientifical approach katika masuala ya kiroho
Mkuu uhakika wa nilichoandika tangu awali unatokana na sehemu husika ya andiko ulilonukuu.
Bahati mbaya kabisa wewe umenyofoa kineno kimoja (uongo) alichotamka Mtume Paulo, ili kumtwika sifa ya kishetani ya uongo.
Nimekuuliza tena na tena swali rahisi ambalo unakwepa kujibu hata robo yake.
Iwapo Mtume anadai yeye ni mwongo, kuna lipi la kumwamini katika yote asemayo?
Pili kwa msingi wa mantiki ya Biblia, Paulo Mtume mwenyewe akikemea mara nyingi kuhusu uongo na waongo plus hukumu itakayowakabili katika kiyama, huoni kwamba wazo lako ni potofu mno?
Hilo hukufanya wewe uonekane unafumbia macho hoja fulani ili kusisitiza hoja nyingine ambayo kimsingi ni duni, isina mantiki yoyote.
Nakariri upya nilichotanabaisha mapema kwamba dhima ya Warumi 3 ni uturufu wa haki ya Mungu ukishabihishwa na hulka ovu ya mwanadamu.
Nanukuu hapa huo mtiririko:
3:3 Je kutoamini kwa Wayahudi kutaubatilisha uaminifu wa Mungu?
[Mtume hapa anauliza: Is it possible? Jibu lake katika andiko linalofuata]
3:4 Hasha! Mungu na aonekane mkweli hata kama
kila mtu awe mwongo...
[Hapa unaweza kuona wapi itokapo ile dhana ya ^uongo wangu^ anayojizungumzia Mtume katika andiko la 3:7]
3:5 Lakini ikiwa
udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini?....]
[Katika andiko la 4 Mtume Paulo anatumia maneno ^kila mtu awe mwongo^ na hapa katika andiko la 5 anatumia maneno ^udhalimu wetu,^ kusudi likiwa lilelile la kuzipambanua dhana hizi na haki ya Mungu. Ndivyo pia ilivyo katika andiko la 7.]
3:7 Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu Wake kwa sababu ya
uongo wangu...
Unaweza kuona wazi kwamba kwenye haya maandiko matatu (3:4, 5 na 7) kimetangulia kipengele cha unadharia (hypothetical element):
3:4
though everyone were a liar (ESV)
3:5 But
if our unrighteousness serves to show...
3:7 But
if through my lie...
Sasa tunahitimishaje? Kamwe katu Mtume Paulo hasemi yeye ni mwongo.
Kwa sababu hilo halikubaliani na uhalisia wa utume wake na hata fundamental principles za basic reasoning.
Yeye ni Mtume wa Mungu na anena kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.
Vilevile kukubali dhana hiyo kunafanya ujumbe wote na mantiki nzima ya Mtume viwe batili - siyo tu potofu bali visivyoeleweka kwa vile vinajipinga vyenyewe.
Kwa mara ya elfu nadhani, nauliza tena, kama Mtume anadai yeye ni mwongo kimtazamo wako huoni kwamba hapo hapaswi kuaminika kwa lolote - ikiwa ni pamoja na kauli hiihii kwamba yeye ni mwongo?
Mwisho, andiko la Warumi 3:7 Mtume Paulo anajinasibia ubinadamu kama ilivyo 3:4 na 3:5 ili kupambanua na kuthibitisha haki ya Mungu.
Msingi wake hasa uko katika 3:3 ^Vipi kama baadhi yao hawakuwa waaminifu? Je kutoamini kwao kwaubatilisha uaminifu wa Mungu?^
Ni wazi maandiko yanayofuata Mtume anajenga hoja za kufafanua mantiki hii.