Hii ushajibiwa."Samahani, nilikwisha kukuambia kwamba nitakudanganya,"
kisha akakukabidhi Biblia na kukuomba usome Warumi 3:7:
“Lakini ikiwa kwa uongo wangu kweli ya Mungu imezidi kudhihirika kwa utukufu wake, mbona mimi bado nihukumiwe kama mwenye dhambi?” (Warumi 3:7)
Sasa utakuwa na udhuru gani? Je, unaweza kufikiria sababu yoyote?
Mwenye kujua muktadha wa ushahidi wa Warumi 3:7 tafadhali ajitokeze kunusuru kondo za Bwana zisije kuingia jahanamu bila kujua.
otherwise, Nyie wafuasi wa Paulo jifikirie sana Paulo sio mtu wakutegemea ndo chanzo cha Utatu ambao hata Yesu hakuufundisha.
Mkuu sawa umeeleza vizuri ila umekosa kuleta hata ushahidi hata ya mfano sisi tutakuelewa je?au si kama yale yale ya Paulo bila ushahidi hoja yako haija kama sawa.Mkuu hiyo inaitwa illustrative hypothetical situation - hali nadharia fafanuzi.
Ni kielelezo chenye lengo la kutanabaisha mantiki ya ukweli kuhusu haki ya Mungu.
Mtume Paulo anajenga hoja yake kuhusu uturufu wa haki ya Mungu kwa kuonesha namna inavyothibitika kwenye udhaifu wa mwanadamu.
3:5 anatumia mfano wa ^uovu wetu^
3:7 anatumia mfano wa ^uongo wangu^
Hamaanishi anayosema ni uongo, bali anajitwika uhusika wa ubinadamu kwa ujumla - ubinadamu ambao kiasili ni wenye dhambi.
Kama Paulo anamaanisha kwamba yeye ni muongo, sasa twawezaje hata kuamini chochote asemacho - pamoja na ujumbe husika katika andiko hili?
Nani kanijibu mkuu, nahitaji majibu yenye ushahidi sio ngojera tu na hadeeth kama za Paulo.Hii ushajibiwa.
Usirudie rudie hoja
Tena mkuu don't confuse wanachama wa Jf tafadhali Kupunguza hoja ya Paulo kuwa "hypothetical" si sahihi muktadha mzimaMkuu hiyo inaitwa illustrative hypothetical situation - hali nadharia fafanuzi.
Ni kielelezo chenye lengo la kutanabaisha mantiki ya ukweli kuhusu haki ya Mungu.
Mtume Paulo anajenga hoja yake kuhusu uturufu wa haki ya Mungu kwa kuonesha namna inavyothibitika kwenye udhaifu wa hulka ya mwanadamu.
3:5 anatumia mfano wa ^uovu wetu^
3:7 anatumia mfano wa ^uongo wangu^
Hamaanishi mambo asemayo ni uongo, bali anajitwika uhusika wa ubinadamu kwa ujumla - ubinadamu ambao kiasili ni wenye dhambi.
Kama Paulo anamaanisha kwamba yeye ni muongo, sasa twawezaje hata kuamini chochote asemacho - pamoja na ujumbe husika katika andiko hili?
Nani kanijibu mkuu, nahitaji majibu yenye ushahidi sio ngojera tu na hadeeth kama za Paulo.
Waje wajitetee hapa hao wòte ni viazi hawana intellectual capability ya kujibu hoja sawa waje tuwasikilize sasa tena kama wana la kusema la maana yasiwe matusi na kuvamia imani nyingineHii hoja ilifafanuliwa vizur tu na bro hamis77 pamoja na Meneja Wa Makampuni.
Mkuu hoja yako inaibua mtanziko wa mantiki (logical paradox) kumhusu Mtume Paulo.Tena mkuu don't confuse wanachama wa Jf tafadhali Kupunguza hoja ya Paulo kuwa "hypothetical" si sahihi muktadha mzima
Warumi 3:1–8 sio tu "hali ya nadharia" pekee, bali ni mazungumzo yenye maswali na majibu (diatribe). Paulo anatumia mtindo huu mara nyingi ili kujibishia hoja ambazo tayari zilikuwapo dhidi ya injili yake (mfano pia 1 Wakorintho 15:35, Warumi 9:19). Hivyo, kusema "ni mfano tu" haimalizi tatizo, kwa kuwa maandiko bado yanabaki yakisema wazi: “kwa uongo wangu...”
Mkuu masuala ya kiroho au spritual to a large extent logic is not applicable, huenda roho mtakatifu alipitia kwa njia hiyo kutaarifu ummah wanao mfuata Paulo, kwasbabu alibuni mengi, kama architecture wa modern christianity, Mungu katuma roho mtakatifu kufanya Paulo mwenyewe kua shahidi mwenyewe kwenye uongo wake alio tunga.... so don't be too scientifical in that case, ukienda hivo tutahoji mengiMkuu hoja yako inaibua mtanziko wa mantiki (logical paradox) kumhusu Mtume Paulo.
Unaamini Mtume Paulo hapa anajithibitisha kwamba ni mwongo?
Halafu ili iweje? Halafu nani amwamini kwenye mengine yote asemayo?
Hebu pima mambo kwa basic reasoning kwanza.
Usiruke na jambo hewani alimradi tu linasomeka na kuandikika.
Unachodai kifilosofia kinaitwa perfomative contradiction (ukinzani wa kiutendaji) ambapo maudhui ya kauli fulani inapingana na uasili wa kauli yenyewe.
Ndiyo maana nimekuuliza iwapo Mtume Paulo alimaanisha hilo usemalo kwamba ni mwongo, sasa tumwamini katika lipi lolote?
Mtu akidai yeye ni mwongo, maana yake nyingine ni kwamba hata kwa kauli hii hajasema kweli.
Implication? Aweza kuwa mwongo au vinginevyo - yaani haaminiki kwa lolote.
Umedai ametumia mtindo wa mahojiano katika uwasilishaji wake.
Kwani hali nadharia fafanuzi (illustrative hypothetical situation) haiwezi kutumia namna ya maswali na majibu?
Je umewahi kusoma kitabu cha Ayubu - ambapo anawauliza watesi wake kuhusu maswali yanayolenga kuifafanua mantiki yake - japo ni vielelezo tu?
Unasema to a large extent & huenda?Mkuu masuala ya kiroho au spritual to a large extent logic is not applicable, huenda roho mtakatifu alipitia kwa njia hiyo kutaarifu ummah wanao mfuata Paulo, kwasbabu alibuni mengi, kama architecture wa modern christianity, Mungu katuma roho mtakatifu kufanya Paulo mwenyewe kua shahidi mwenyewe kwenye uongo wake alio tunga.... so don't be too scientifical in that case, ukienda hivo tutahoji mengi
Sasa mkuu tusipo tumia "huenda" wewe unawakikika bila kuleta ushahidi wa maandiko kwamba tafsiri yako kuhusu hilo la Paulo kua muongo? probability sentence ni lazima itumike paka pale utakopo bainisha kwamba Paulo alitumia lugha ya mafumbo kumanisha hilo aliko sema, ila otherwise tutachukua maneno yake kama yalivo kwasbabu na maneno ya bibulia yote huchukiliwa hivo hivo..... wewe unaleta scientifical approach katika masuala ya kirohoUnasema to a large extent & huenda?
Hivi umegundua kwamba to a large extent haiondoi ukweli nilioubainisha hapo juu?
Kadhalika, nakukumbusha kwamba huenda maana yake huna hakika.
Unazidi kujichanganya mno ukidai Roho Mtakatifu alinena na Mtume Paulo kwa kumjaza uongo.
Ni wazi hujui Roho Mtakatifu ni nani. Nakushauri sana ukasome Yohana 14 hadi sura ya 16 ili upate mwanga japo kidogo kuhusu hilo.
Lastly, nakukumbusha kwamba kila kauli ya kweli lazima iwe logical and reasonable (mantikifu na maanifu).
Pia logic lazima iwe na msingi wake - ama ni general speaking, biblical speaking, etc.
Katika logical speaking tunajiuliza kama kauli fulani ina-make sense, inafuata reasonable thinking, inashabihi kanuni za clear reasoning?
Kwa bahati mbaya kabisa unacholazimisha Warumi 3:7 iseme kinapishana na kupingana kukubwa mno na hata vile viwango vya chini zaidi vya kipimo hiki kuhusu basic reasoning.
Ndiyo kusemaje? Unaweza kulazimisha Biblia iseme utakavyo, lakini hiyo haina maana kwamba ndilo kusudi tarajiwa la andiko husika.
Mkuu uhakika wa nilichoandika tangu awali unatokana na sehemu husika ya andiko ulilonukuu.Sasa mkuu tusipo tumia "huenda" wewe unawakikika bila kuleta ushahidi wa maandiko kwamba tafsiri yako kuhusu hilo la Paulo kua muongo? probability sentence ni lazima itumike paka pale utakopo bainisha kwamba Paulo alitumia lugha ya mafumbo kumanisha hilo aliko sema, ila otherwise tutachukua maneno yake kama yalivo kwasbabu na maneno ya bibulia yote huchukiliwa hivo hivo..... wewe unaleta scientifical approach katika masuala ya kiroho
Kwenye maandiko haya ya Paulo kuna tatizo la mkanganyiko wa hoja kwa sababu anajenga nadharia tata (hypotheticals) bila kutoa msimamo wa moja kwa moja.Mkuu uhakika wa nilichoandika tangu awali unatokana na sehemu husika ya andiko ulilonukuu.
Bahati mbaya kabisa wewe umenyofoa kineno kimoja (uongo) alichotamka Mtume Paulo, ili kumsingizia kwamba yeye ni mwongo.
Nimekuuliza tena na tena swali rahisi ambalo unakwepa kujibu hata robo yake.
Iwapo Mtume anadai yeye ni mwongo, kuna lipi la kumwamini katika yote asemayo?
Pili kwa msingi wa mantiki ya Biblia, Paulo Mtume mwenyewe akikemea mara nyingi kuhusu uongo na waongo plus hukumu itakayowakabili katika kiyama, huoni kwamba wazo lako ni potofu mno?
Hilo hukufanya wewe uonekane unafumbia macho hoja fulani ili kusisitiza hoja nyingine ambayo kimsingi ni duni, isina mantiki yoyote.
Nakariri upya nilichotanabaisha mapema kwamba dhima ya Warumi 3 ni uturufu wa haki ya Mungu ukishabihishwa na hulka ovu ya mwanadamu.
Nanukuu hapa huo mtiririko:
3:3 Je kutoamini kwa Wayahudi kutaubatilisha uaminifu wa Mungu?
[Mtume hapa anauliza: Is it possible? Jibu lake katika andiko linalofuata]
3:4 Hasha! Mungu na aonekane mkweli hata kama kila mtu awe mwongo...
[Hapa unaweza kuona wapi itokapo ile dhana ya ^uongo wangu^ anayojizungumzia Mtume katika andiko la 3:7]
3:5 Lakini ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini?....]
[Katika andiko la 4 Mtume Paulo anatumia maneno ^kila mtu awe mwongo^ na hapa katika andiko la 5 anatumia maneno ^udhalimu wetu,^ kusudi likiwa lilelile la kuzipambanua dhana hizi na haki ya Mungu. Ndivyo pia ilivyo katika andiko la 7.]
3:7 Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu Wake kwa sababu ya uongo wangu...
Unaweza kuona wazi kwamba kwenye haya maandiko matatu (3:4, 5 na 7) kimetangulia kipengele cha unadharia (hypothetical element):
3:4 though everyone were a liar (ESV)
3:5 But if our unrighteousness serves to show...
3:7 But if through my lie...
Sasa tunahitimishaje? Kamwe katu Mtume Paulo hasemi yeye ni mwongo.
Kwa sababu hilo halikubaliani na uhalisia wa utume wake na hata fundamental principles za basic reasoning.
Yeye ni Mtume wa Mungu na anena kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.
Vilevile kukubali dhana hiyo kunafanya ujumbe wote na mantiki nzima ya Mtume viwe batili - siyo tu potofu bali visivyoeleweka kwa vile vinajipinga vyenyewe.
Kwa mara ya elfu nadhani, nauliza tena, Mtume anadai yeye ni mwongo huoni kwamba hapo hapaswi kuaminika kwa lolote - ikiwa ni pamoja na kauli hiihii kwamba yeye ni mwongo?
Mwisho, andiko la Warumi 3:7 Mtume Paulo anajinasibia ubinadamu kama ilivyo 3:4 na 3:5 ili kupambanua na kuthibitisha haki ya Mungu.
Msingi wake hasa uko katika 3:3 ^Vipi kama baadhi yao hawakuwa waaminifu? Je kutoamini kwao kwaubatilisha uaminifu wa Mungu?^
Ni wazi maandiko yanayofuata Mtume anajenga hoja za kufafanua mantiki hii.
Warumi 3:4 inasomeka vizuri hivi:Kwenye maandiko haya ya Paulo kuna tatizo la mkanganyiko wa hoja kwa sababu anajenga nadharia tata (hypotheticals) bila kutoa msimamo wa moja kwa moja.
Warumi 3:4 “Kila mtu awe mwongo”
Hapa Paulo anasema kana kwamba uongo wa wanadamu ni jambo linalothibitisha haki ya Mungu. Hii inaleta swali: kama uongo wa wanadamu unadhihirisha uaminifu wa Mungu, je, basi uongo si sehemu ya mpango wa Mungu?
Warumi 3:5 “Lakini ikiwa udhalimu wetu unaonyesha haki ya Mungu, tutasema nini? Je, Mungu ni dhalimu kwa kuleta ghadhabu?”
Hapa Paulo mwenyewe anakiri swali la mantiki linalotokea: Kwa nini Mungu atuadhibu kwa dhambi zetu ikiwa dhambi hizo zinamsaidia kuonekana mwenye haki? Hata anajaribu kuliondoa swali hili haraka kwa kusema “nasema kwa jinsi ya kibinadamu” kana kwamba ni hoja ya kupita.