Je Jaji Mkuu anaweza kukamatwa na Askari?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Watu wa Sheria naombeni jibu, Jaji Mkuu anaweza kukamatwa na Askari wetu na kufikishwa Mahakamani? Najua Raisi wa nchi hawezi kukamatwa, vp kuhusu Jaji Mkuu?
 
Kama atakuwa na makosa ya kushitakiwa na ikabidi akamatwe na polisi basi anakamatwa.
 
Kwani katika nchi hii ukiondoa Rais wa JMT ni nani tena mwenye kinga ya kutoshitakiwa?
 
kuanzia kwa makamu wa rais hadi mwenyekiti wa kitongoji kisheria wote ni nyanganyanga. Lazima wakumbwe na msukomsuko
 
Kwa kosa gani kuwa precise,kuwa anaweza kukamatwa kwa tuhuma fulani? Maana jaji mkuu ana privilege na immunity......na kukamatwa sio kirahisi ivyoo........toa scenario yako vizuri mkuu
 
Kwa mtazamo wangu... Jaji mkuu atakamatwa na polisi ila kwa amri ya raisi na sio mtu mwengine.. ata kama ata tenda kosa, kitakacho tokea ni raisi kumvua madaraka na kuwa km mm na ww yaani raia wa kawaida hapo ndio atahukumiwa ila sio akiwa km jaji mkuu.. lazima amri itoke kwa raisi .. ndio maana hata wenzetu kenya uhuru amesema lazima atadili na jaji mkuu akipata uraisi ... Wote wako chini ya raisi na chini ya raisi ndio kuna polisi. Ni mtazamo wangu tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…