Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?
Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.
Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.
Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.
Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.
Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukumbi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.
Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
Mkuu japo Uzi ni wa muda mrefu, tangu 2009, Nadhani bado ninayo nafasi kuchangia, ili wanachama wenzagu ndani ya JF, wapate kujua ni kwa nini natumia jina/id ya ya Mgodo visa.
Ilikuwa ni 1992, nakumbuka nilikuwa moja ya Madarasa (ningeomba nisitaje) katika shule ya Msingi Kibasila.
Kwa ufupi, nilikuwa ni mtu wa Story nyingi za Vituko na Matukio, nilikuwa ni moja ya watu wachekeshaji na nisie kaukiwa na Vibweka (yote hii ilisababishwa na Mzee wangu kumiliki Runinga mapema).
Siku moja katika Maongezi, ilitokea ndani yake badala ya kutamka neno MDOGO, mimi nikatamka MGODO...
Basi hapo ndipo kama jina lilizaliwa.
Kila mmoja anajua, pale unapo jifanya mjuaji, na bahati mbaya UKACHAPIA..
Jina lilinibamba, watu Mgodo...Mgodo..na wengine wakaongezea neno Visa.. (likazaliwa Mgodo visa)
Bahati nzuri/mbaya nikaenda/nikachaguliwa Elimu ya Sekondari, shule moja na baadhi ya class mate, jina Mgodo visa likaendelea...kutokana na kuendelea na Vituko au mbwembwe.
Wanafunzi wengine wakaona jina hilo limekaa mahala pake....yaani acha tu wana JF, Jina langu halisi, mpaka ndugu zangu wenyewe wameshaa lisahau..but life goes on, jina ni utambulisho tu, no matter ni zuri au baya.
Ndio maana yupo na MASUDI KIPANYA..