Kwa urembo wa umbo, shape, sura, waist line, bust line, leggy line, nywele, shingo, macho na miondoko, Wahangaza ndio wanaongoza, wameumbwa wakaumbika, wanatazama na kutazamika ila sijawahi kubahatika nao katika mbambo mengine.
Uzuri uko wa aina nyingi, uzuri wa mke ni tabia, uzuri wa mahitaji ni performance, na uzuri wa machoni ni kuona, inategemea uzuri gani unaoutaka wewe, kama ni ule uzuri wa kufurahisha macho, mbona wazuri kibao tuu tunawaona, wengi wala hawaolewi, wao kutwa kucha wanahangaika wakitanga na njia huku wapenzi wao macho juu juu, lakini kuna wazuri wa ndani kwa uzuri usiionekana, hao ndio hao wameolewa, waume zao wanapata raha na maisha yanasonga!