Je, kama Taifa, ikigundulika kwamba ama tunaficha au tunatoa takwimu zisizo sahihi kuhusu janga la COVID-19, tunaweza kuwajibishwa kimataifa?

Je, kama Taifa, ikigundulika kwamba ama tunaficha au tunatoa takwimu zisizo sahihi kuhusu janga la COVID-19, tunaweza kuwajibishwa kimataifa?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Ziko taarifa kuwa upo uchunguzi unaoendelea kuhusu tuhuma kuwa China kwa makusudi ama ilizembea au ilizuia utoaji wa taarifa sahihi kuhusu chanzo na kuenea kwa coronavirus pamoja na idadi ya vifo vilivyotokana na janga hilo.

Ikiwa tuhuma hii itathibitishwa, kuna uwezekano wa China kuchukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kutengwa na hata kushtakiwa kwa kukiuka makubaliano ya kimataifa kuhusu mlipuko hatari kama huu wa COVID-19.

Je, katika hali kama hii Tanzania itapona?
 
Kwa Sasa Hakuna namna Tena ambyo Serikali inaweza kutoa taarifa sahihi hasa za Vifo vya korona. Watu wanajifia ovyo baada ya maambukizi ya ndani kuwa makubwa kwa sababu ya uzembe wa serikali na kupenda mapato. Na ikitokea Serikali inaweza kutoa taarifa sahihi, dunia utashangaa why Tanzania Tena Afrika
 
Ziko taarifa kuwa upo uchunguzi unaoendelea kuhusu tuhuma kuwa China kwa makusudi ama ilizembea au ilizuia utoaji wa taarifa sahihi kuhusu chanzo na kuenea kwa coronavirus pamoja na idadi ya vifo vilivyotokana na janga hilo. Ikiwa tuhuma hii itathibitishwa, kuna uwezekano wa China kuchukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kutengwa na hata kushtakiwa kwa kukiuka makubaliano ya kimataifa kuhusu mlipuko hatari kama huu wa COVID-19.

Je katika hali kama hii Tanzania itapona?
Sisi tutaanza kuwajibishwa na majirani zetu kwanza, tena wataanza kututenga.

Tulijigamba kwamba sisi tunategemewa na majirani nane, kwa hiyo hatuwezi kufunga mipaka yetu. Sasa wameanza wao kukataa madereva wetu kwenda kwao. Kama haukuwa unafiki kujigamba kuwa tunategemewa, na sasa hao hao tuliowasemea wanatusuta, itakuwa ni kitu gani hicho.

Kimataifa kiujumla, tukizidiwa sana, mataifa hayatuacha tuangamie kabisa. Watatuokota na kutunywesha uji hata kama ni kwa lazima.
Ila huu utawala uliochanganyikiwa kabisa unaweza ukalazimishwa kukaa pembeni ikiwa kama sharti la uji huo.

Litakuwa jukumu letu kama nchi, baada ya hapo kuamua ni nini kifanyike kwao kutokana na uchafuzi huu wanaolifanyia taifa letu.
Naona kama 'meltdown' inawaandama kiasi cha kuchanganyikiwa wasijue wafanye nini wakati mambo yakizidi kubomoka.

Hata huo uchumi waliodhani wanaulinda kwa maamuzi yao ya ajabu, hawaonyeshi kufanya wala kusema chochote juu yake. Wamebaki tu kumwachia Mungu kwa zile sala walizohimiza.

Je, Mungu amezikataa sala zao?
 
Ki nchi kama cha kwetu kama unahatarisha afya ya dunia, ingelikuwa Reagan, anakupiga mabomu! Kwa sasa ni ngumu! Trump ndiyo hivyo ni takataka!
 
Ofcourse sisi tunakwamisha juhudi za dunia nzima katika kupambana na hili janga kwa sababu ya kiburi tu na ulevi wa madaraka!.

Kabla hata ya kushitakiwa tutakuwa blacklisted na Mataifa kwa kuhatarisha usalama wao.

Tulichokifanya TZ cha kuruhusu watalii kuingia nchini wakati dunia imechafuka na kisha kukataa kuchukua jitihada za kuzuia huu ugonjwa usisambae nchi nzima ni kitendo cha watu wanaoangalia pafupi sana.

Lakini let me tell you one thing, Corona hii haitoishia kwetu sisi tu akina baba Kabwela, Itapiga familia zao na wao wenyewe hapo ndo watajua how shortsighted they were!
 
Ziko taarifa kuwa upo uchunguzi unaoendelea kuhusu tuhuma kuwa China kwa makusudi ama ilizembea au ilizuia utoaji wa taarifa sahihi kuhusu chanzo na kuenea kwa coronavirus pamoja na idadi ya vifo vilivyotokana na janga hilo. Ikiwa tuhuma hii itathibitishwa, kuna uwezekano wa China kuchukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kutengwa na hata kushtakiwa kwa kukiuka makubaliano ya kimataifa kuhusu mlipuko hatari kama huu wa COVID-19.

Je katika hali kama hii Tanzania itapona?
Jibu sahihi ni kuwa hatutapona.......
 
Wewe hata bila corona kama hauna ubavu na haukubaliani na wenye ubavu dunia hii unaweza kuwajibishwa tu.

"You are either with us or you're against us".

Una nini wewe wanachokihitaji wenye ubavu wanyime uone kama hautowajibishwa!
 
Mag3,

..nadhani china hataadhibiwa.

..ila sina uhakika kama Dr.Tedros atadumu ktk nafasi yake.

..naona US watamfanyia figisu mpaka aondoke kama ilivyotokea kwa Dr.Boutrous Ghali.
JokaKuu anayemfanyia figisu Dr. Tedros ni kichaa moja tu, Donald Trump na Wamarekani walio wengi hawamuungi mkono. Kumbuka ushahidi upo kwamba awali Trump alimsifia sana Rais wa China. Ili kujinusuru ndio akamrukia Dr. Tedros.
 
Ila akili zingine ngumu kuamini hasa kwa kiongozi mkubwa sijui haangalii TV international news,hasa also kuwaambia watu ni fursa mlimani mihogo na mazao mengine,tumieni vizuri mvua kipindi hiki cha corona inaunyama hapa bado hakuna lockdown mtakufa njaa mkachape kazi
 
Back
Top Bottom