Ziko taarifa kuwa upo uchunguzi unaoendelea kuhusu tuhuma kuwa China kwa makusudi ama ilizembea au ilizuia utoaji wa taarifa sahihi kuhusu chanzo na kuenea kwa coronavirus pamoja na idadi ya vifo vilivyotokana na janga hilo. Ikiwa tuhuma hii itathibitishwa, kuna uwezekano wa China kuchukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kutengwa na hata kushtakiwa kwa kukiuka makubaliano ya kimataifa kuhusu mlipuko hatari kama huu wa COVID-19.
Je katika hali kama hii Tanzania itapona?
Sisi tutaanza kuwajibishwa na majirani zetu kwanza, tena wataanza kututenga.
Tulijigamba kwamba sisi tunategemewa na majirani nane, kwa hiyo hatuwezi kufunga mipaka yetu. Sasa wameanza wao kukataa madereva wetu kwenda kwao. Kama haukuwa unafiki kujigamba kuwa tunategemewa, na sasa hao hao tuliowasemea wanatusuta, itakuwa ni kitu gani hicho.
Kimataifa kiujumla, tukizidiwa sana, mataifa hayatuacha tuangamie kabisa. Watatuokota na kutunywesha uji hata kama ni kwa lazima.
Ila huu utawala uliochanganyikiwa kabisa unaweza ukalazimishwa kukaa pembeni ikiwa kama sharti la uji huo.
Litakuwa jukumu letu kama nchi, baada ya hapo kuamua ni nini kifanyike kwao kutokana na uchafuzi huu wanaolifanyia taifa letu.
Naona kama 'meltdown' inawaandama kiasi cha kuchanganyikiwa wasijue wafanye nini wakati mambo yakizidi kubomoka.
Hata huo uchumi waliodhani wanaulinda kwa maamuzi yao ya ajabu, hawaonyeshi kufanya wala kusema chochote juu yake. Wamebaki tu kumwachia Mungu kwa zile sala walizohimiza.
Je, Mungu amezikataa sala zao?