Je Kamati iliyomuadhibu Hajji Manara ni tofauti na ile iliyomuadhibu kocha wa makipa Mashujaa FC?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kocha wa makipa Mashujaa FC kampiga kocha wa Mbeya City wazi wazi bila ya kificho na dunia imeona.

NALIA NGWENA nimeshangazwa sana na hiyo adhabu ndogo aliyopewa lakini Hajji Manara aliyekua msemaji wa Yanga kabla ya kufungiwa alibishana na Raisi wa TFF tu Tena kwa ushahidi wa kubangaiza lakini kapigwa nyundo ya miaka na faini ya shilingi milioni 20.

Sasa Najiuliza hizi kamati zinazoratibu adhabu huwa zinaangalia watu kwanza usoni au Kuna kanuni zinafatwa au zinakomoa watu makusudi??

Kamati ya adhabu TFF fanyeni kazi kwa kufuata kanuni na Wala siyo kuangalia sura na kumkomoa mtu.
 
Ngoja waje kukupa jawabu la swali lako, lakini jibu la kwanza watakwambia ni kwa kuwa Manara amekuwa na makosa ya kujirudia rudia... Mimi napita tu[emoji188]
 
Hii ni thread ya pili haitaji adhabu yenyewe as if wote tumeisoma hio adhabu! Why mnatupa adhabu ya kutoa mawazo yetu Kwa njia ya ramli? Wekeni adhabu tajwa
 
Nalia Ngwena mpira wa bongo una madudu mengi,kocha wa Mbeya aende mahakamani kumshtaki yule mwehu wa Mashujaa.
 
Bado una Imani na soka la Bongo?

Bado una Imani na TFF.

Bado una Imani na stars.

Bado una Imani na Budget za Simba na yanga....

KICHWA CHAKO KITAKUWA HAKIPO SAWA.
 
wametos adhabu ndogo sana kwa huyo kocha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…