Je, kampuni mbili zinaweza kusajiliwa chini ya kampuni moja?

Je, kampuni mbili zinaweza kusajiliwa chini ya kampuni moja?

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
21,600
Reaction score
35,158
Naomba mnieleweshe.

Kama mtu anataka fungua kampuni A na B ina maana lazima awe na bank acc mbili na kila moja ifanye kazi kivyake.

Je, inawezekana hizi kampuni mbili zika sajiliwa chini ya kampuni moja? Mfano badala ya kuwa na kampuni A na B ukawa na kampuni C na hii kampuni C iwe na hizo kampuni A na B?

Je, nini faida ya kuwa na kampuni mama? Je, nikiwa na kampuni mama italazimisha kila kampuni ndogo ziwe na mahesabu yake? Acc yake benki?

Naomba mwongozo!
 
Inawezekana mfano AZAM GROUP OF COMPANY ndani yake ina utitili wa kampuni ndogondogo km unavyoona SAMSUNG ni GROUP OF COMPANY ambapo ana mpk kampuni ya vipodozi kutengeneza injini za magari n.k

N.B mimi sio mtaaramu ni mganga tu wa kienyeji hila SERIEZ za KIKOREA ndio zimenipa maujanja mengi ya maswala ya biashara makampuni mambo ya share horder n.k
 
Aisee
 
Mkuu,hili swali sikuliona ila naweza kulijibu hata leo kama bado hujapata jibu.

JIBU ni NDIO kampuni inaweza kuanzisha kampuni, kumiliki hisa katika kampuni na hata kuuza kampuni. Swali la kujiuliza je, ni kwa nini niwe na kampuni ndani ya kampuni? Sababu ziko nyingo lakini kubwa ambalo unapaswa kufahamu ni kujilinda na kulinda mali zako. Matajiri wengi huwa na holding company na wengine hata huanzisha TRUST lengo likiwa kulinda mali zao.

Katika maswala ya kikodi kila kampuni inao wajibu wa kulipa kodi.Usimamizi na uendeshaji wa masuala ya kodi unategemea hisa malengo, muundo na mfumo wa uendeshaji wa kampuni.

Kwa mfano unaweza kuanzisha HOLDING Company ambayo yenye haifanyi TRADING ya aina yoyote ile kisha hizo kampuni Tanzu zenyewe zikahangaika na masuala yake ya kibiashara na kikodi yenyewe au unaweza kuanzisha kampuni hodhi ambayo itawajibika na masuala ya kodi yote. Lengo lako ndo litaamua kampuni yako iwe katika muundo gani. IWE ni Subsidiary, Branch.

So mkuu ndio unaweza.
 
Back
Top Bottom