Mkuu,hili swali sikuliona ila naweza kulijibu hata leo kama bado hujapata jibu.
JIBU ni NDIO kampuni inaweza kuanzisha kampuni, kumiliki hisa katika kampuni na hata kuuza kampuni. Swali la kujiuliza je, ni kwa nini niwe na kampuni ndani ya kampuni? Sababu ziko nyingo lakini kubwa ambalo unapaswa kufahamu ni kujilinda na kulinda mali zako. Matajiri wengi huwa na holding company na wengine hata huanzisha TRUST lengo likiwa kulinda mali zao.
Katika maswala ya kikodi kila kampuni inao wajibu wa kulipa kodi.Usimamizi na uendeshaji wa masuala ya kodi unategemea hisa malengo, muundo na mfumo wa uendeshaji wa kampuni.
Kwa mfano unaweza kuanzisha HOLDING Company ambayo yenye haifanyi TRADING ya aina yoyote ile kisha hizo kampuni Tanzu zenyewe zikahangaika na masuala yake ya kibiashara na kikodi yenyewe au unaweza kuanzisha kampuni hodhi ambayo itawajibika na masuala ya kodi yote. Lengo lako ndo litaamua kampuni yako iwe katika muundo gani. IWE ni Subsidiary, Branch.
So mkuu ndio unaweza.