Je, kampuni za bima za vyombo vya moto zinasaidia vipi kufanya wamiliki kuwa makini barabarani?

Je, kampuni za bima za vyombo vya moto zinasaidia vipi kufanya wamiliki kuwa makini barabarani?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
motor insurance 1.jpg

Bima za vyombo vya moto zimekuwa msaada mkubwa kwa watu wanaotumia vyombo hivi hasa ikitokea chombo chako kimehusika kwenye ajali.

Lakini je, kampuni za hizi za vyombo vya moto hapa nchini zinachangia vipi kufanya wanaomiliki vyombo vya usafiri siyo tu kuendelea kutumia huduma zao bila matatizo yoyote lakini kuwa watu ambao wanapunguza ongezeko la ajali nchini?

Mfano dereva amekuwa mteja wenu kwa miaka kumi au kumi na tano na hajawahi kupata ajali hata mara moja, mnafanya nini kumhamasisha dereva huyu kuendeleza umakini barabarani na kuendelea kuwa dereva bora?

Mnampa motisha gani ambayo itamhamasisha yeye kuendelea kuwa bora zaidi lakini hata hawa wanao legalega wakahamasika kutia jitihada katika kuendesha vyombo vyao?

Wadau masemaje?​
 
Back
Top Bottom