Kwanza tujiulize "Kampuni" ni nani?
Kampuni ni legal person kisheria, yaani Kampuni anaweza kumiliki property, kuingia mkataba, kukopa, nk kama mtu wa kawaida anavyoweza.
Linapokuja suala la kumkopesha kampuni, mabenki huwa wanamfanyia kampuni assessment juu ya kiwango cha mkopo na pia kama anao uwezo wa kulipa huo mkopo kwa kuangalia financial statements za huyo kampuni.
Kwenye financial statements za kampuni tutaona mali anazomiliki, madeni alokua nayo mpaka sasa na pia mtaji aliokua nao. Vilevile tutaweza kuona faida anayotengeneza kila mwezi, na gharama zake za uzalishaji au uendeshaji.
tukijiridhisha kuwa kampuni ana hali nzuri ya kifedha (ataweza kulipa mkopo), basi tutampatia huo mkopo. akishindwa kulipa baadae tutampeleka mahakamani, mahakama itam-declare bankruptcy kisha mali za kampuni zitauzwa ili kuwalipa watu wanaomdai.